Filamu yenye mapito ya Celine Dion mbioni kuachiwa

Filamu yenye mapito ya Celine Dion mbioni kuachiwa

Mwanamuziki Celin Dion amezua gumzo mitandaoni baada ya trela ya filamu yake ikimuonesha akilia kwa uchungu wakati akielezea mapito yake kufuatia na ugonjwa unaomsumbua wa ‘Stiff Person Syndrome’ uliomuanza mwaka 2022.

Kwa mujibu wa tovuti ya ‘The Sun’ imeeleza kuwa licha ya Dion kujipa mapumziko ya muda lakini alikuwa akishirikiana na Amazoni kurekodi filamu yake iitwayo ‘I Am: Celine Dion’ inayotarajiwa kutoka Juni 25 mwaka huu.

"Nimegunduliwa na ugonjwa wa nadra sana wa neva na sikuwa tayari kusema chochote hapo awali lakini niko tayari sasa.

"Siyo ngumu kufanya onesho, ni ngumu kughaili onesho, alisema huku akitokwa na machozi, ninafanya kazi kwa bidii kila siku lakini lazima nikubali, imekuwa ngumu, nimewakosea sana watu, ikiwa siwezi kukimbia, nitatembea. Ikiwa siwezi kutembea, nitatambaa lakini sitaacha, kufanya nianacho kipenda,”amesema.

Ikumbukwe kuwa Desemba 2022 Celine Dion alitangaza kuwa na ugonjwa adimu ambao hauna tiba kupitia ukurasa wake wa Instagram huku akilazimika kughailisha ziara yake ya dunia.

Filamu yake hiyo ni njia ya kuonesha vita yake na ugonjwa huo ambao haujulikani sana kwa umma, kulingana na tangazo la Amazon, filamu itafichua yale yote yaliyokuwa nyuma ya pazia wakati wa mapambano ya kutafuta tiba ya ugonjwa huo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags