Filamu ya Diddy inayohusu kesi, kuoneshwa hivi karibuni

Filamu ya Diddy inayohusu kesi, kuoneshwa hivi karibuni

Filamu iliyoandaliwa na 50 Cent kuhusu madai ya unyanyasaji wa kingono yanayomkabili Diddy, iitwayo ‘Diddy Do It?’ inatarajiwa kuoneshwa katika mtandao wa Netflix hivi karibuni.

Kwa mujibu wa tmz Netflix iko hatua za mwisho kupata hati ya kuonesha filamu hiyo iliyotayarishwa kwenye studio za Cent, ‘G-Unit’ baada ya kuzipiga chini baadhi ya Tv na mitandao iliyokuwa ikitaka kuionesha filamu hiyo kwa mara ya kwanza.

50 Cent akijibu kuhusu habari hiyo kupitia ukurasa wake wa Instagram ameeleza kuwa ili Netflix iweze kujihakikishia kuonesha filamu hiyo inabidi waathiriwa wajitokeze kwa wingi ili kuweza kupata vipindi zaidi.



Ikumbukwe kuwa habari ya filamu ya Diddy kuoneshwa Netflix inakuja muda mfupi baada ya kusambaa kwa video ikimuonesha Combs akimshambulia mpenzi wake wa zamani Cassie Ventura katika hoteli ya Los Angeles mwaka 2016.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags