Fifa yamfungia kinara wa mabao Afcon 2023

Fifa yamfungia kinara wa mabao Afcon 2023

Shirikisho la kimataifa la vyama vya soka (Fifa) limesisitiza kwamba aliyekuwa kinara wa mabao kwenye fainali za Afcon 2023, Emilio Nsue, hakupaswa kuichezea timu ya taifa ya Equatorial Guinea kwa muda wake wote wa miaka 11 aliyotumikia kwenye soka la kimataifa.

Desemba 2013, Fifa ilisema Nsue hakuwa na ruhusa ya kuichezea Equatorial Guinea kwa kuwa aliichezea timu ya vijana ya Hispania kwenye mechi za kimataifa, lakini alipuuza na kuendelea kuichezea timu ya taifa ya nchi hiyo ya Afrika Magharibi.

Uchunguzi mpya ulifanyika Machi 2023 kuangalia kama Nsue anastahili kuichezea Equatorial Guinea kwenye soka la kimataifa, ambapo mshambuliaji huyo alipewa siku sita za kujibu tuhuma hizo.

Fifa alisema: “Hakukuwa na majibu yoyote kutoka kwa mtuhumiwa.”

Na taarifa ya Fifa iliyotolewa Jumatatu ilifichua kwamba Equatorial Guinea itavuliwa ushindi wao iliyopata kwenye mechi ya kufuzu Kombe la Dunia 2026 dhidi ya Namibia na Liberia, ambapo wapinzani wao wamepewa pointi tatu na ushindi wa mabao matatu. Mechi zote hizo, Equatorial Guinea ilishinda 1-0 na mabao hayo yalifungwa na Nsue.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags