Fid Q: Hip Hop zamani, ya sasa haina jipya

Fid Q: Hip Hop zamani, ya sasa haina jipya

Mkongwe wa muziki wa HipHop hapa nchini Farid Kubanda maarufu kama Fid Q, anayetamba na ngoma kama Propaganda, Kibiriti, Ripoti za Mtaani, Sumu, Champion na nyingine nyingi , amefunguka suala zima kuhusiana na Hip hop ya sasa kutokuwa na jipya.

Fid Q akizungumza na Mwanaspoti ameeleza kuwa Hip hop ya sasa haina jipya kutokana na uwasilishwaji wake.

“Ni wazi bado muziki wa hip hop wa zamani umedhihirisha kuwa na impact zaidi kuliko huu mpya kwasababu ya maudhui na style zilizotumika kwenye uwasilishwaji wake, wasanii wa zamani walikua unique kwasababu kila mmoja alikua na style yake isiyofanana na mwingine na wengi walikua wakiwakilisha ( kisanaa ) wanapotoka, kiasi kwamba ukisikia “ Afande Sele “ kimoyomoyo unasema Morogoro ndani ya nyumba “ au ukisikia “ Fid Q “ unakua unapata picha ya Mwanza”

“Nguvu hii na nyingine zisioni kwa hawa wapya. Na hata kimapokeo.. wasanii wa zamani walifanikiwa kufikisha sanaa yao kwenye sehemu kubwa ya jamii, wa siku hizi ni kama wanafanya sanaa kwa ajili ya kugusa au kufurahisha kikundi fulani cha watu wachache” amesema Fid Q

Mbali na hayo alifunguka kuhusu namna anavyoona ushindani wa muziki huo kwa sasa na kudai kuwa haoni ushindani wa kisanaa bali anaona ushindani katika kufanya promo za kazi.

“Mimi sioni ushindani wa kisanaa ninauona ushindani wa kipromosheni au kwa lugha nyepesi kiuwekezaji.. yaani ule wa nani ana hela ya kulipia online promo au kuweka muziki kwenye YouTube ads ( muziki unakua unajitokeza kama tangazo bila kuutafuta) ili uweze kuwafikia wengi”

“Kwa ufupi siku hizi ukiwa na hela ya kupush mziki.. unaweza kutengeneza hit song.. na ndio maana kuna tofauti kati ya best song na hit song, yaani sio kila hit song ni best song na sio kila best song inaweza kuhit”, amesema Fid Q






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags