Felix Auger bingwa wa tennis Rotterdam Open 2022

Felix Auger bingwa wa tennis Rotterdam Open 2022

Felix Auger -Aliassime amekuwa bingwa wa mashindano ya Tennis ya Rotterdam Open ya Nchini Uholanzi baada ya kumfunga mgiriki Stefano Tsitsipas anayeshika nafasi ya nne kwenye viwango vya ubora Duniani kwa seti 2-0.

Felix (21) anayeshika nafasi ya tisa kwenye viwango vya ubora Duniani ameshindwa kwa 6-4, 6-2 katika mchezo uliodumu kwa dakika 78. Ushindi huo ni wa kwanza kwa nyota huyo baada ya kupoteza fainali 8 mfululizo.

Baada ya Ubingwa huo, Felix amesema “Ni siku ya furaha sana kwenye maisha yangu ya Tennis na ninaimani ni mwanzo wa makombe mengi yanayokuja” amesema

Nyota huyo raia wa Canada alitabiriwa makubwa baada ya kuwatoa vigogo wa England, Cameroon Norrie na Andy Murray kwenye michezo ya hatua za mwisho za mtoano wa mashindano hayo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags