Fei Toto sasa ni mali ya Azam Fc

Fei Toto sasa ni mali ya Azam Fc

Alooooooh! Baada ya sakata la kijana mwenye mashuti yake mjini, hatimae uongozi wa Yanga SC umetangaza kumalizana na mchezaji Feisal Salum maarufu kama 'Fei Toto' ambaye rasmi wamemuuza klabu ya Azam FC.

Katika taarifa iliyotolewa na timu hiyo imeeleza dau ambalo ameuzwa halitawekwa wazu kutokana na makubaliano ya pande zote mbili.

“Feisal ataungana na timu yake mpya baada ya makubaliano binafsi na dirisha la usajili kufunguliwa rasmi”

Uwiiii! Haya wadau wangu kujeni hapa, unategemea kuona jambo gani jipya kutoka kwa Fei Toto katika msimu ujao, dondosha komenti yako hapo chini mwanangu sana.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags