FDA imependekeza kupiga marufuku bidhaa za kunyoosha nywele

FDA imependekeza kupiga marufuku bidhaa za kunyoosha nywele

Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini Marekani imependekeza kupiga marufuku bidhaa za kunyoosha nywele kutokana na masuala ya kiafya.

Mamlaka hiyi inasema kuwa inapendekeza kupiga marufuku haswa bidhaa za kunyoosha nywele ambazo zina kemikali zinazotoa formaldehyde kama vile methylene na glycol kwani kwa miaka mingi, wanasayansi wamekuwa wakihusisha mtumizi ya kemikali hizo na magonjwa ya saratani.

Kwa mujibu wa FDA imedai kuwa suala hilo linaathiri hasa wanawake weusi kwani asilimia 50 ya bidhaa zilizo huuzwa kwa wanawake weusi kwani wao ndiyo wengi hutumia kufanya nywele zao zinyooke.

FDA inaeleza athari mbaya za kiafya zinazoweza kupatikana ni kama vile shida ya kupumua na saratani, huku wakitaja bidhaa hizo ni pamoja na dawa za nywele na vifaa vya kunyooshea.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags