Fat Joe: Chris Brown asingejihusisha na mapenzi angekuwa kama MJ

Fat Joe: Chris Brown asingejihusisha na mapenzi angekuwa kama MJ

‘Rapa’ mkongwe kutoka nchini Marekani, #FatJoe amedai kuwa #ChrisBrown asingejiingiza kwenye mapenzi angekuwa kwenye kiwango sawa na marehemu #MichaelJackson.

Joe ameyasema hayo kupitia podcast yake ya ‘The Biggest Fat Joe’, kwa kueleza kuwa Chris Brown asingejiingiza kwenye migongano ya kimapenzi na Ex wake Rihanna angekuwa kama MJ kwa sababu ni mwanamuziki mwenye kipaji kikubwa katika kizazi hiki.

“Kama Chris Brown asingeingia kwenye ugomvi na Rihanna, tungekuwa tunamwita Michael Jackson sasa hivi. Yeye ndiye mwanamuziki mwenye talanta zaidi kwenye wakati wetu. Hakuna wa kumkaribia” alisema Fat Joe

Utakumbuka Februari 8, 2009 Chris Brown alimshambulia kimwili aliyekuwa mpenzi wake Rihanna tukio ambalo lilipelekea wawili hao kuachana na kuingia katika ugomvi mkubwa.

Fat Joe mwenye umri wa miaka 53 amekuwa akitamba na ngoma zake kama ‘All The way Up’, ‘Lean Back, Fat Joe Speaks’, ‘SunShine’, ‘Flow Joe’ na nyinginezo.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags