Fashion tips kwa wanawake wenye matiti madogo na makubwa

Fashion tips kwa wanawake wenye matiti madogo na makubwa

Hellow mambo vipi watu wangu wa nguvu karibu sana kwenye ukurasa wa fashion kama kawaida ndiyo sehemu pekee ya kujidai na kupangilia mionekano yetu au sio?

Wiki hii bwana kwenye kipengele hiki tutazungumzia  Tips za fashion kwa wanawake wenye matiti madogo na makubwa jinsi gani wanatakiwa kuvaa ili kuboresha mionekano yao.

Jarida la Mwananchin scoop limepata fursa ya kufanya mahojiano na Fashion disagner anayetambulika kwa majina Elizabeth Paul ambaye anapatikana Sinza palestina.

Akizungumza na mwandishi wa Makala haya Elizabeth ameeleza kuwa watu wanatofautiana maumbo kwani wapo wenye matiti madogo lakini wanamatumbo makubwa halkadhalika wapo wenye matiti makubwa na wanatumbo pia.

watu wenye matiti madogo wanatakiwa kuvaa nguo za namna gani ili waweze kupendeza zaidi.

Inasidikika kuwa watu wenye matiti madogo wanamapana sana ya uchaguzi wanguo kwani kuna uwezekano mkubwa sana kwa wao kupata mavazi mazuri popote pale ukilinganisha na wenye matiti makubwa huwa ni tofauti.

“Kwenye fashion mimi kama disagner kazi yangu kubwa ni kuhakikisha kila mtu kulingana na muonekano wake aweze kupendeza kulingana na mwenyewe alivyo.”amesema Elizabeth

Akielezea wanawake wenye matiti ama vifua vidogo wanapendeza sana wakivaa colourfull dresses yaani nguo zenye shaning colours kwani ni nguo ambazo zina more attention.

Wanawake wenye matiti madogo pia wanashauriwa kuvaa nguo ambazo ni poolneck zinawafaa kwa namna ambayo vifua vyao vinakua vidogo tofauti na mwenye matiti makubwa akivaa hivyo anaweza kuwa kituko.

Hata hivyo amesema uzuri wa kuvaa pool neck unaweza kuvalia na suruali, sketi au hata bwanga na unaweza kupendeza pia.

Accessories

Mtu wenye matiti madogo anashauriwa pia kupendelea kuvaa accessories kutokana na attraction yake inakua kifuani mwake kuanzia kwenye mabega.

“Kutokana na watu wa aina hii wanakua hawana zile nyamanyama za kwenye mabega kwahiyo akivaa accessories wanakua wanapatamore attention”amesema Elizabeth

Aidha aliongeza kuwa mwanamke huyo anapendeza pia zaidi akivaa nguo ambazo zinamshape hata kama ikimbana kuanzia juu hadi chini anapendeza kutokana na anakua hana zile nyamanyama za tumbo.

Off shoulder dress

Wanawake wenye matiti madogo wanashauriwa pia kuvaa nguo ambazo ni offshoulder zinampendeza kutokana na anakua hajajaa sana hivyo anauwezo wa kuvaa bila sidiria.

Vilevile anapendeza akivaa nguo za katamikono kwasababu zinamfanya awe nadhifu zaidi kulingana na maumbile yake kuanzia kifuani hadi kwenye mikono.

NOTE: watu wenye matiti madogo attention zao hua zinakua tumboni yaani kuanzia kwenye bega hadi chini ya titi.

Fahamu kuwa mtu mwenye matiti makubwa akivaa nguo ambazo zina belt anapendeza na kuvutia zaidi kwani zinamtengenezea shape vizuri na inatenganisha kati ya tumbo na ziwa.

Mtu wenye matiti makubwa hashauriwi kuvaa accessories kwasababu attention yake sio kifuani kwani tayari kifua chake kinakua kimejaa.

“Anatakiwa kuvaa rough dress yaani gauni za kuzungusha ambazo zinamsaidia yeye ku adjust kifuani tofauti na akivaa nguo zenye vifungo kwani inawezakutokea kifungo kikatatuka muda wowote hivyo anashauriwa kuvaa nguo ambazo hazina vifungo”anasema

Hata hivyo anashauriwa kuvaa two pieces yaani blauzi na suruali, aublauzi na bwanga,blauzi na sketi kwani zitamsaidia kutengeneza shape vizuri.

Halkadhalika pia anashauriwa kuvaa nguo ambazo zina shingo aina ya V kwani zitamsaidia pia kuweka muonekano mzuri kwenye kifua chake kwani hashauriwi kuvaa poolneck ataonekana kama amevimbamba kutokana na kifua chake kilivyo.

“Anashauriwa zaidi kuvaa nguo ambazo ni cool colours na sio shouting colours  ambazo rangi zinakua zimepoa hupendeza zaidi japo inategemea na rangi ya mtu” anasema na kuongeza

“Kutokana na tabia mbalimbali za watu wenye matiti makubwa kwani sio mara nyingi lakini inasadikika kuwa inaweza ikatokea mchoro kati ya kwapa na titi haukai vizuri pindi akitokwa na jasho ule mchoro unaweza kujitokeza hadi kwenye chuchu kwahiyo akivaa cool colour inaweza kumsaidia pia kwenye un necessary yoyote ile ambayo inaweza kutokea ya kimaumbile.”alisema.

Woow!! I hope fashion wiki hii nimekukuna vilivyo mtu wangu kwa mada mbalimbali na uchambuzi juu ya masuala ya fashion usipitwe na jarida la Mwananchi scoop kila Ijumaa thank you tukutane next week!!.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags