Familia yataja sababu kifo cha Costa Titch

Familia yataja sababu kifo cha Costa Titch

Familia ya aliyekuwa mwanamuziki na dancer kutoka Afrika Kusini marehemu #CostaTitch wametoa taarifa rasmi ya sababu ya kifo cha mwanamuziki huyo.

Tovuti ya The Express Tribune imeeleza kuwa kutokana na uvumi unaoendelea kuhusu kifo cha msanii huyo familia yake imeweka wazi sababu ya kifo chake ambapo kulingana na majibu ya uchunguzi kutoka kwa mtaalamu wa magonjwa maalumu ya (Human tissue’) Costa Titch alipata mgandamizo mkubwa katika moyo wake.

Mtaalamu huyo amefafanua hali hiyo ambayo haikujulikana ilianza lini kwa Costa ambayo ilisababishwa na msongo wa mawazo, uchovu wa muda mrefu na kupelekea mapigo ya moyo kwenda kwa kasi isivyo kawaida.

 Hayo yaligunduliwa baada ya uchunguzi wa maiti ya mwanamuziki huyo ambaye alikuwa mkali wa Amapiano nchini.

Ikumbukwe kuwa mwamuziki huyo alifariki March 11 mwaka jana baada ya kupata mshtuko na kudondoka akiwa jukwaani alipokuwa akitumbuiza katika tamasha la ‘Utra Music’ nchini Africa Kusini.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags