Familia ya Diddy mahakamani kuomba dhamana

Familia ya Diddy mahakamani kuomba dhamana

Familia ya mwanamuziki wa hip hop Marekani, Diddy ikiingia Mahakamani kwa ajili ya kuomba dhamana kwa mara ya tatu.


Kwa mujibu wa Fox News wanasheria wa Diddy wamepeleka tena ombi la kuomba dhamana huku wakiwa na fedha taslimu dola milioni 50 hata hivyo hakimu anayesimamia kesi ya Combs hajatoa uamuzi wowote mpaka sasa huku akiwataka kuwasilisha nyaraka zao ifikapo Jumatatu Novemba 25,2024.


Kwa sasa Diddy amezuiliwa katika jela ya MDC Brooklyn baada ya kukataliwa dhamana kwa zaidi ya mara mbili huku jaji anayendesha kesi yake akidai kuwa Combs hawezi kuachiwa huru kwani serikali inaamini mshatakiwa ni hatari kwa jamii.

Ikumbukwe Diddy alikamatwa na kutupwa gerezani Septemba 16 jijini Ney York kwa makosa makubwa ya unyanyasaji wa ngono, usafirishaji haramu wa watu huku kesi yake ikianza kusikilizwa Me 5, 2025.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags