Faiza Ally: bado nampenda Sugu

Faiza Ally: bado nampenda Sugu

Moja ya kati ya story inayobamba katika mitandao ya kijamii ni ya mwanadada Faiza Ally ambaye amefunguka na kusema kuwa bado anampenda mzazi mwenzake Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu.

Faiza amesema kuwa alimpenda sana Sugu na hajawai kumchukia hata siku moja na amekuwa akijaribu kumuona mbaya lakini hakufanikiwa katika hilo.

“Sitakuwa tayrai kwa namna yoyote kuvunja mahusiano ya baba Sasha ya ssa hivi aliyoyajenga lakini kumjulisha mtu kuwa unampenda na wala umchukii sio dhambi, na najua anaelewa kuwa kama nampenda na nasema kuwa siwezi kuja kumchukia na siku zinavyozidi kwenda nakuwa mkubwa zaidi hivyo siwezi kuweka kitu rohoni,” alisema

Hata hivyo Faiza alisema bado hawajakaa katika mstari mzuri na baba watoto wake lakini hali ya sasa ni nafuu kuliko ilivyokuwa zamani.

“Hatujakaa kwenye mstari mzuri lakini binti yangu amekua uhitaji kuongea na baba yake kusema anahitaji nini hivyo wakati mwingine tunangea baba mtoto wangu wakati mwingine hatuongei lakini sio mbaya kama ilivyokuwa zamani,” alisema Faiza

 

 


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post