Faini yamnyemelea Haaland kwa kumkashifu muamuzi

Faini yamnyemelea Haaland kwa kumkashifu muamuzi

Mchezaji wa ‘klabu’ ya #ManchesterCity, #ErlingHaaland, huenda akapigwa faini na FA baada ya kumkashifu muamuzi #SimonHooper kufuatia sare ya 3-3 dhidi ya ‘klabu’ ya #TottenhamHotspur, siku ya Jumapili, Novemba 3.

Haaland alikasirika baada ya muamuzi kushindwa kuruhusu mpira uendelee kwa kumpa faida Grealish ambaye mbali ya kufanyiwa madhambi bado alikuwa akiendelea kucheza.

Baada ya mchezo kumalizikia, Hooper alizingirwa na wachezaji wa City, huku Haaland akidhihirisha hasira yake kwenye mtandao wa X na kutumia lugha chafu ambayo huenda FA wakamfungulia mashtaka ya utovu wa nidhamu.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags