Faida za kuwa na mipaka kwenye mahusiano kabla ya Ndoa

Faida za kuwa na mipaka kwenye mahusiano kabla ya Ndoa



Habiba Mohamed

Niajeeee niajeee!watu wa nguvu,Ebwana katika kona yetu ya  mahusiano tunaangalia faida ya kuwa na mipaka kwenye mahusiano kabla ya ndoa.

Kama inavyojulikana mahusiano ama uchumba ni hatua ya kwanza kabla ya kuingia kwenye ndoa na katika hatua hiyo kuna mambo kadhaa muhimu kwa wapenzi kuyazingatia ikiwemo mipaka katika mahusiano namna gani mnavyoishi au kuyaendesha mahusiano yenu.

Wanasaikolojia na wataalamu wa mahusiano wanasema kuna faida ya kuwa na mipaka kabla ya ndoa nazo ni;-

  • Kuwa na mipaka katika mahusiano kuna saidia kuwa na uhuru katika kuchagua kipi kilichosahihi na kipi sio sa hihi kwa mwenza wako,kama inavyojulikana mahusiano ni hatua ya kwanza katika kuelekea ndoa hivyo hakuna sheria au utaratibu unaokufunga katika kuchagua unachokipenda au kilichosahihi.
  • Kuwa na mipaka katika mahusiano kuna kusaidia kufanya uamuzi uliosahihi kwa kuchuja mienendo ya mpenzi ulinaye na malengo mlionayo kwa miaka ya mbeleni na kutunza utu wako .
  • Pia inasaidia kujua tabia ya mwenza wako kwa mfano muda anaompatia mwenza wake,kujali,heshima na utu maana wapenzi wengi wanaonyesha tabia nzuri kwa wenza wao wakiwa karibu au Pamoja.
  • Vilevile inasaidia kuonyesha umiliki au wajibu kama mpenzi wako anatimiza wajibu kwa mpenzi wake.

Aiseeeeeeee!mahusiano yana vitu vingi na bado tunaendelea kujifunza dondoo za wanasaikolojia,Haya  mwanangu wa faida shusha comment yako hapo chini utueleze kwenye mahusiano yako uko na mipaka gani  na mwenza wako? Au ndo wale wanitumie nauli na kuila?






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags