Faida ya wafanyakazi kujifunza huduma ya kwanza

Faida ya wafanyakazi kujifunza huduma ya kwanza

Na Aisha Lungato

Katika maisha ya kawaida mambo hatari yanayoweza kusababisha mtu kupoteze maisha ni pale anapokosa msaada wa huduma ya kwanza pindi anapokabiliwa na ugonjwa au madhara ya ghafla.

Kama inavyofahamika ugonjwa humkuta mtu yeyote. Mwananchi Scoop tumekusogezea umuhimu wa wafanyakazi kujifunza huduma ya kwanza, kwani kazini ni sehemu ambayo watu mbalimbali hukutana na kila mmoja huwa na matatizo yake.

Kutokana na hili kuna haja kwa waajiri kutoa elimu kwa wafanyakazi wao kuhusiana na huduma ya kwanza. Ni wazi kuwa suala hili limekuwa likizungumzwa mara kadhaa na watalaamu wa afya, serikali na wanaharakati lakini ukweli ni kwamba bado halijapewa uzito wake katika maeneo mengi nchini.

 

Elimu ya huduma ya kwanza ni muhimu, hivyo ni vyema kila ofisi kuzingatia kwani kuokoa maisha, kupunguza maumivu, kuzuia hali ya mgonjwa isizidi kuwa mbaya pia husaidia kuharakisha uponaji kabla ya mgonjwa kupata matibabu hospitalini.

Vitu vya kufanya kuonesha umuhimu wa huduma ya kwanza

  • Ofisi kutoa elimu kwa wafanyakazi wake

Ofisi ama shirika linatakiwa kutoa semina kwa wafanyakazi wake ambapo semina hii inaweza kufanyika mara moja kwa wiki au mara mbili ili kuepusha kuchukua muda wa kufanya kazi.

  • Wafanyakazi kuzingatia Afya zao

Ili kuepukana na matukia ya dharura inabidi wafanyakazi kucheaki afya zao mara kwa mara, yapo matukio ya dharura ambayo hayatokani na ugonjwa lakini mengi yanakuwa ni yale ambayo yamesababisha na muhusiaka mwenyewe.

  • Ofisi au taasisi kuwafanyia cheak up wafanyakazi wake.

Kuwafanyia cheak up wafanyakazi kutasaidia kupunguza matukio ya dharura kwani itamsaidi mtu binafsi kujua anatatizo gani na kwa jinsi gani anaweza kulihendo ili lisilete taharuki mbele za watu.

  • Ofisi husika kununua box lenye vifaa vya huduma ya kwanza

Kutoa mafunzo ni hatua ya kwanza na hatua ya pili ni kununua First aid kit kwa ajili ya kuwasaidia watu watakapota matatizo

 

  • Ofisi iajiri dokta au nesi

Kama ilivyo katika shule na sehemu zingine, inabidi kwenye ofisi mbalimbali kuwepo na wauguzi ili litokeapo tatizo iwe rahisi kutoa msaada.

Licha ya hayo mamlaka kuhisika chini ya Wizara ya Afya inatakiwa kuanzisha mafunzi maalum ambayo yanatoa elimu katika masomo ya vyuo vikuu.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags