Faida ya vyama vya wafanyakazi

Faida ya vyama vya wafanyakazi

Nawasalimu kwa jina la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Kazi iendelee, najua kabisa huko mtakuwa mmeitikia kimoyo moyo wanangu sana, sasa hapa namaanisha kazi iendelee haswaa na leo katika segment yetu tupo na kitu pambe haswaa.

Swala la vyama vya wafanyakazi limekuwa changamoto kwa waajiriwa katika sehemu zao za kazi, sasa Mwananchi Scoop katika Makala ya kazi tunaekuelezea umuhimu wa vyama vya wafanyakazi katika maeneo ya kazi.

Kulingana na sheria ya ajira na mahusiano ya kazi chama cha wafanyakazi ni idadi yoyote ya wafanyakazi inayohusiana pamoja kwa madhumuni, ikiwa kipekee au kwa madhumuni mengine ya kusimamia mahusiano kati ya wafanyakazi na waajiri wao,

Aidha mashirika ya waajiri ambayo waajiri wao ni wanachama vilevile ili vyama vya wafanyakazi viweze kutimiza majukumu yake lazima muajiri akubali uwepo wa vyama hivyo katika shirika au kampuni yake na ikiwa na sheria na kanuni zilizopo pia vyama hivi ni hiari kujiunga na sio lazima.

 

Kwa ilivyo zoeleka vyama vya kazi vinavyo tambulisha waajiri hujulikana kama TUCTA (Trade union congress of Tanzania) na wajiriwa hutambulishwa na TUGHE (Tanzania Union of Government of Health Employees).

Na huu ndio umuhimu wa vyama vya wafanyakazi katika kampuni au taasisi yoyote.

 

  • Vyama vya wafanyakazi ni kutetea na kulinda maslahi ya wafanyakazi kwa waajiri wao, kwani chama humtambulisha mfanyakazi katika majadiliano ili kupata stahiki bora kazi mfano maswala ya likizo (martenity leave, sick leave) na ongezeko la mishahara.

 

  • Kutoa elimu kwa waajiri na wafanyakazi kuhusiana na afya na usalama katika mazingira ya kazi kwa mfano taasisi ya (OSHA) pia kuboresha uhusiano wao katika mahali pa kazi.

 

  • Inaongeza ushirikiano na umoja kati ya mwajiri na mfanyakazi katika ufafanuzi wa sheria elekezi za nchi ili kuboresha utendaji wao wa kazi na ufanisi na tija ili kuwepo na urahisi katika uandaaji wa mikataba ya hali bora.

 

  • Husaidia kupunguza migogoro katika eneo la kazi kati ya mwajiri na mwajiriwa kupitia sheria za vyama zilizopo zinazo muongoza mujiari.

 

Hata hivyo licha ya vyama vya wafanyakazi kuwa na umuhimu katika mahali pa kazi vilevile vina jukumu la kuhamasisha usawa wa jinsia katika maeneo ya kazi na kutoa kipaumbele kwa sekta zisizo rasmi kujiunga na kuunda vyama vya wafanyakazi katika kute






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post