Faida na hasara za wivu kwenye mahusiano

Faida na hasara za wivu kwenye mahusiano

Na Habiba Mohamed

Helow Niaje  niajeeeee! Mapenzi  yanatawala dunia,Mapenzi ndo tatizo linalozungumzwa kila siku basi kama kawaida  naendelea kukupa maujanja uweze kufurahi na umpendae na mapenzi yenu Yazidi kuwa ya motooo.

Wanasaikolojia wanasema wivu ni chakula cha nafsi,moja kati ya mahojiano yaliyofanywa na mwanasaikolojia mashughuri Cosmas Madulu anasema kuwa wivu unahitajika sana katika mahusiano, mmoja wapo katika mahusiano akiwa hana wivu kwa mwenzie basi ana tatizo la kisaikolojia lakini ukizidi pia ni hatari kwa wahusika,"wivu ni chakula cha nafsi ambacho kinamfanya mwanadamu kujihisi yuko salama. Faida ya kwanza inamfanya mtu kuwa salama, wanaume wana shida ya macho ya kupenda kila kitu kizuri wanachokiona kwahiyo anahitaji mwanamke ambaye atamfanyia wivu ili amuweke salama", amesema Madulu.

 

Pia ameongeza kuwa faida ya pili ya wivu ni kuleta heshima katika mahusiano au ndoa. Vilevile katika mahusiano wivu  una hasara kubwa kama ukizidi katika mahusiano, amesema, "wivu ukipitiliza unapelekea mauaji, mtu anaweza kutenda jambo ambalo hakutarajiwa kutokana na akili yake kufunikwa na hisia kubwa. Napenda mfahamu pia lugha 5 za mahusiano ambazo ni maneno matamu, kutumia muda pamoja", ameongeza.

 

Aidha amemalizia kwa kuzitaja silaha kubwa mbili ambazo  mwanamke atazitumia, atadumisha mahusiano dhidi ya mwenza wake kwa kuitumia vizuri masikio yani kusikiliza anachoambiwa na mpenzi wake na sio watu wanayosema pia kuitunza Ngozi yake ili kubaki na mvuto.

Aiseeeee! Kwa wale wenzangu wanaosema kuonyesha wivu kwa mpenzi wako ni udhaifu  sio kwelii bhana tunapoteza silaha ya kulinda mahusiano .Dondosha comment yako utueleze wivu katika mahusiano yako umekusaidia kuboresha penzi au kuharibu?

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags