Faida na hasara za kusoma kozi mtandaoni ukiwa chuoni

Faida na hasara za kusoma kozi mtandaoni ukiwa chuoni

Oooooh! Amkeni amkeni wanangu wa mavyuoni basi bwana kuna wale wavivu kuamka asubuhi kwenda kuwahi lecture huwa wengi wetu tunakimbilia kusoma katika mitandao, sasa tumekusogezea faida na hasara za kusoma mtandaoni ungana nasi kujua Zaidi.

Masomo ya mtandaoni yamekuwepo kwa muda mrefu, lakini hapo mbeleni mfumo huu ulitumika sana sana kufunzia masomo ya postgraduate, yaani akina Masters na PhD.

Ni baada ya corona kufika ndio sasa umekumbatiwa na vyuo vingi vya masomo ya juu kufundishia wanachuo wote, ikiwemo undergraduates. Kwenye vyuo vingi sasa, mfumo wa kufundishia ni blended learning, yaani mchanganyiko wa kusoma uso kwa uso na kusomea mtandaoni. Vipindi vinagawanywa kuna vile mnaenda darasani na vingine mnasoma mtandaoni.

Ni njia rahisi sana ya kuhudhuria na kushiriki vipindi. Kama huna experience na online learning, unaweza dhani inakuwaga na complicated process, ama haiko as efficient as kuenda darasani physically.

Ndivyo nilidhani hadi nilipohudhuria kipindi cha kwanza cha mtandaoni. Kwa kweli process ni rahisi sana ya kuingia na kuchangia. Unachihitaji ni laptop na Wi-Fi connection, lakini hata simu na data inawezatosha.

Platform zinazotumika ni kadhaa; inawezakuwa Google Meet, ama Zoom, ama platform ya chuo chenu. Kwa kozi za mtandaoni ambazo sio za chuo, huwa wanavideo zao zimerekodiwa kabisa ukijiunga tu kusoma unawza kuziangalia na hivyo kusoma kupitia hizo. Lakini hata zikiwa nyingi zinafanana mambo mengi, hivyo si tatizo. Kwenye kipindi mwalimu anawezakushea screen yake kila mtu akaweza kuona anachofundisha, unawezawasha microphone kuuliza swali, na pia wewe unawezakushea screen yako kupresent kwenye darasa. Ni rahisi hivyo.

Unaweza pia kurekodi kipindi hicho ili ukakipitie baadaye, ingawaje wahadhiri wengi tayari hurekodi na kuweka vipindi hivyo mtandaoni, labda kwenye portal ya shule ili wale ambao hawakuweza kuhudhuria wapate kilichofundishwa. Lakini kama mwalimu wenu harekodi, unaweza jifanyia mwenyewe.

Faida za kusomea mtandaoni

  • Hakuna kwenda darasani. Hii haswa husaidia watu ambao wanakaa mbali na shule. Kama kipindi kinaanza saa moja asubuhi, huna haja ati kuamka saa kumi na mbili ili ujitayarishe upande basi ufike shule. Unaweza amka dakika kumi kabla, uoshe uso na kwa click tatu tayari uko darasani. Unasave muda ambao ungetumia kusafiri, na hela za nauli pia. Muda huo unaweza utumia kuextend usingizi ama kusoma.
  • Unaweza kurekodi lecture ukaipitia baadaye.
  • Kwa maoni yangu, unapata nafasi nzuri ya kufuatilia kinachofundishwa. Kama ni notes ambazo mwalimu anatumia au picha ambazo anazieleza, unaona vizuri kabisa kwenye screen yako bila kustrain, ukilinganisha na inavyokuwa darasani wakati mwingine, labda kama unakaa mbali na ubao na presentation na huoni vizuri ama humsikii mwalimu vizuri.
  • Unaweza kusoma muda wowote, na sehemu yoyote. Iwe usiku, mchana, usiku wa manane nk
  • Mwalimu ana uhuru wa kutumia resources nyingi kufunndishia. Anaweza fungua video ama browser akasearch kitu na kuwaonesha kwa urahisi, kitu ambacho hakingewezekana darasani.

Hasara za masomo ya mtandaoni;

  • Vipindi  vingine haviko suited kwa masomo ya mtandaoni. Kwa mfano hesabu na vipindi kama hivyo ambavyo mwalimu anafundisha calculations huwa afadhali vikifanyiwa darsani uso kwa uso.
  • Kama huna discipline ya kuwa makini darasani unaweza kuwa distracted na mambo mengine kama simu ama ukaenda kubrowse vitu vingine wakati kipindi kinaendelea. Masomo ya mtandaoni yanahitaji uweze kuwa makini, sana sana kwa vile mwalimu hayuko karibu kukuangalia ukifanya mambo yako.

Haya sasa wanangu sana natumai mmeelewa kuhusiana na swala zima la kusoma mtandaoni kama unavyoona hapo tumekujuza mbivu na mbichi so uamuzi ni wako waswahili wanakamsemo kao bwana utaamua kunyoa au kusuka chamuhimu Zaidi ni kutoboa na kuvaa joho hahha ama nini watu wangu wa nguvu. Tuishi humoo

 


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post