Fahamu undani wa kitabu chenye kurasa 128 zisizoandikwa kitu

Fahamu undani wa kitabu chenye kurasa 128 zisizoandikwa kitu

Inafahamika kuwa watu hutafuta vitabu kwa ajili ya kusoma na kuongeza maarifa kulingana na aina ya maudhui yaliyomo ndani ya kitabu husika.

Waandishi wengi wamekuwa wakiandika vitabu kwa hali ya ustadi wa kutumia maneno mengi yenye kuvutia wasomaji ili waendelee kusoma.

Lakini hiyo ni tofauti kwa kitabu kiitwacho “Everything Men Know About Women” kwani kitabu hicho kina zaidi ya kurasa 100 lakini zote zipo wazi kwani hazijaandikwa kitu chochote.

Kitabu hicho kwa mara ya kwanza kiliandikwa mwaka 1988 na muandishi Dr. Alan Francis  na hadi kufikia mwaka 2013 vitabu takribani 1.5 milioni vilikuwa vimenunuliwa.

Na inaelezwa kuwa kuachwa wazi kwa vitabu hivyo kulikuwa kwa makusudi kabisa ikiwa na maana ya kuwa hakuna kitu ambacho wanaume wanajua kuhusu wanawake.

Bali jinsia zote zinatakiwa kuwa na muda wa kusikilizana na kuulizana maswali ili kufanya uhusiano uweze kudumu na kuelewana zaidi.

Pamoja na hayo kitabu kimoja kinauza kwa zaidi ya tsh 100k.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags