Fahamu tamasha la kupigana makonde ili kumaliza migogoro

Fahamu tamasha la kupigana makonde ili kumaliza migogoro

Ukistaajabu ya Mussa utayaona ya Firauni, hivi ndivyo unaweza kusema kutokana na njia wanayotumia jamii ya Santo Tomás kutoa hasira zao na kutatua migogoro.

Jamii ya Santo Tomás kutoka nchini Peru huandaa tamasha la kitamaduni kwenye uwanja wa michezo kila mwaka ifikapo Desema 25 ambapo watu wenye migogoro hupigana makonde kumaliza tofauti zao.

Lengo la kupigana ni ishara ya kumaliza tofauti zilizotokea mwaka mzima kwa mtu binafsi, rafiki, au mwanafamilia bila kutumia vurugu zaidi au Mahakama.


Kawaida tamasha hilo linaandaliwa na wakazi wa Wilaya ya Chumbivilcas ambapo watu waliokoseana hupigana ngumi.
Sheria ya mapigano hayo hairuhusu kung'ata, kupiga wale walio chini, au kuvuta nywele.

Mshindi huchaguliwa baada ya mmoja kulemewa kwa kipigo na endapo aliyepoteza pambano anapingana na matokeo, anaruhisiwa kukata rufaa kwa pigano lingine.

Aidha, mwanzoni na mwishoni mwa mapigano, wapinzani lazima washikane mikono au kupigana busu ndipo wanaingia ulingoni. Hata hivyo baada ya mapigano hushiriki pombe kwa pamoja na kuanza mwaka mpya bila kinyongo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags