Fahamu siri ushangiliaji wa Messi kunyoosha vidole angani

Fahamu siri ushangiliaji wa Messi kunyoosha vidole angani

Imekuwa kawaida kwa mashabiki wa mpira wa miguu kuvutiwa na ushangiliaji wa baadhi ya wachezaji, kuna wakati mchezaji hupendwa na mashabiki wengi wa kila rika kutokana na aina ya ushangiliaji wake.

Akizungumziwa aliyekuwa mchezaji wa Yanga Feston Mayele watu wengi wanaelewa balaa lake la ushangaliaji alilokuwa akifanya mara tu akitikisa nyavu, jambo ambalo si wakubwa tu bali hata watoto wanaelewa swala la utetemaji wa Fiston.

Fahamu kwamba baadhi ya wachezaji hutumia ishara mbalimbali katika ushangiliaji kufikisha ujumbe fulani, jambo hilo linajionesha kwa mchezaji  maarufu duniani Lionel Messi, ambaye akifunga lazima ashangilie kwa kunyoosha vidole juu angani.

Aina hiyo ya ushangiliji wake imekuwa ikivutia watu wengi, Messi hutumia aina hiyo ya kushangilia akiamini kuwa anatoa salamu za heshima kwa marehemu bibi yake.

Katika moja ya mahojiano aliyowahi kufanya mchezaji huyo  alieleza kuwa kunyoosha kwake vidole juu ni hutoa heshima kwa marehemu bibi yake ambaye ndiye alimpambania kwenye ‘soka’ kwa kumpeleka kwenye shule ya ‘soka’ hadi leo hii ameweza kutimiza ndoto yake ya kuwa mchezaji mkubwa.

Bibi huyo alifahamika kwa jina la Celia Olivera Cuccittini alifariki mwaka 1998, bila kushuhudia matunda ya kipaji cha mjukuu wake aliyekuwa akipambania kumsaidia kukuza kipaji hicho.

.

.

.

#MwananchiScoop

#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags