Fahamu pishi la kuchemsha mayai kwa kutumia haja ndogo nchini China

Fahamu pishi la kuchemsha mayai kwa kutumia haja ndogo nchini China

Duniani kuna tamaduni nyingi, zinazohusisha jamii mbalimbali, wakati huohuo katika jamii husika huziona ni sawa lakini zikienda kwenye jamii yingine watu huziona kama kituko.

Ukizungumzia China kwenye upande wa vyakula utakutana na aina nyingi zipatikanazo nchini humo, ambavyo watu kutoka mataifa mengine hushindwa kuvila na kuviona vya ajabu.

Imezoeleka kuwa watu hutumia maji kuchemsha mayai lakini leo fahamu kuwa nchini China kuna tamaduni ya kuchemsha mayai kwa kutumia haja ndogo ya wavulana walio chini ya miaka 10, ambao bado hawajawahi kushiriki vitendo vya ngono. Mayai hayo huchemshwa na haja ndogo kwa sababu maalumu na hupendwa na watu wengi nchini humo.

Wafanyabiashara wa mayai hayo hutumia mbinu mbalimbali kupata haja ndogo ya kuchemshia kama vile kupeleka madumu ama ndoo kwenye shule za msingi ambazo wanapatikana watoto wenye umri chini ya miaka kumi na kisha hutumia haja hiyo kuchemsha mayai hayo na kisha kuyauza.

Kwa mujibu wa tamaduni hiyo ya China inaelezwa kuwa mayai hayo yanafaida kuliko yale yanayochemshwa kwa kutumia maji, kwani husaidia katika kuboresha mzunguko wa damu, huupa mwili nguvu, huondoa maumivu ya viungo na husaidia kuepukana na kuharusi.

Mayai hayo pia yanasemekana kuwa na harufu nzuri na chumvi, mapishi yake huchukuliwa na kulowekwa kwenye haja kisha baadaye huchemshwa hadi maganda yake yapasuke na huachwa kidogo ili haja ndogo iweze kuingia ndani baada ya hapo hutolewa na kuanza kuuzwa.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags