Fahamu makeke ya Dj mwenye umri mdogo kutoka Afrika Kusini

Fahamu makeke ya Dj mwenye umri mdogo kutoka Afrika Kusini

Suala la wazazi kushiriki katika kukuza vipaji vya watoto wao ni jambo bora zaidi kwani hupelekea  kujenga misingi mizuri kwa watoto tangu wakiwa wadogo kwenye kile wanachopenda kufanya, nchini kuna baaadhi ya wazazi ambao wamekuwa wakishiriki kuhaakikisha vipaji vya watoto wao vinatambulika kwenye jamii na ndiyo maana kuna watoto wanaonekana kwenye tasnia mbalimbali.

Tanzania watoto wengi wanaofahamika ni wale ambao wazazi wao wanaunga mkono vipaji vyao, nchini Afrika Kusini alipatikana Dj mdogo zaidi Duiani anayeitwa Oratilwe AJ Hlongwane, maarufu kama Dj Arch Jnr.

Dj Arch Jnr alianza kuonesha kipaji cha u-dj tangu akiwa na miaka 3, kutokana na wazazi wake kusimamia kipaji chake mwaka 2015 alishinda shindano la South Africa’s Got Talent, ikampelekea mtoto huyo kuvunja record za Dunia za Guiness na kuwa Dj mdogo zaidi Duniani.

Kwa sasa Dj Arch ana umri wa miaka 11, kutokana na kipaji chake ameweza kupata mafanikio mengi ikiwemo, kufungua shule maalum kwa ajili ya kufundisha u-dj kwa watoto na watu wazima wanaopenda kujiunga kwenye darasa lake, kati ya wanafunzi wake ni mdogo wake wa kike ambaye naye anaonekana kufata nyayo za kaka yake.

Dj Arch amewahi kushiriki mashindano mengi ya kusaka vipaji ikiwemo Americas Got Talent, Worlds Got Talent, Britains Got Talent, lakini pia kutokana na kipaji chake amepata wadhamini mbalimbali huku upande wa elimu wazazi wake wameendelea kumsisamia na anadai kuwa ndoto yake nyingine ni kuwa #Pilot.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post