Heyyy! Mambo vipi watu wa nguvu I hope mko powa kabisa kama kawaida yetu huwa hatunaga mba mba mba katika maswala ya kukuhabarisha wewe mfuatiliaji wetu wa Mwananchi Scoop.
Leo katika segmenti yetu ya burudani na michezo, tumekusogezea mchezo ambapo tuseme tuu ukweli unapendwa sana na watu wa nje ya bongo kwasababu kwa hapa bado haujachukuliwa serious sana na hupendwa na watu wa kila rika.
Baseball wengine wanaufahamu kama besibol ni aina ya michezo wa kusisimua sana inayochezwa na timu 2 za watu 9 au 10 ambapo asili yake kubwa ni Marekani ulioletwa na wahamiaji kutoka Ulaya, na mchezo huo tunaweza kuufananisha na kriketi
Mchezo huu huchezwa na timu mbili zinazoshindana kwa shabaha ya kupata ponti zaidi kuliko wengine kila timu huwa na wachezaji 9, zinabadilishana kwa zamu kushambulia na kutetea.
Shabaha ya mchezo ni kuzunguka ("run") uwanja mwenye vituo ("base") nne. Kwa kila mafanikio ya kuzunguka uwanja timu inashika pointi moja. Huku Timu ya wapinzani wanajaribu kuchelewesha na kuzuia wachezaji wa upande mwingine ili wasiweze kupata point na timu yenye pointi zaidi ndio inashinda.
Mchezo wa baseball ukiutazama hivi kwa mara ya kwanza inaweza ikawa ni ngumu kuuelewa kwa jinsi wanavyo cheza lakini ukiendelea kufuatilia kila siku unaweza kuupenda maisha yako yote.
Kama kawaida yangu kunabaadhi leo ndo wanajua kuwa kuna mchezo wa namna hii either anaujua lakini haelewi chochote basi mimi leo ntakujuza ungana name mwanzao mpaka mwisho.
Mchezo wa baseball unachezwa kwenye jukwaa maalum na unachezwa saa kuanzia saa2 hadi 3
Kwa kifupi sheria za kucheza mpira huu au mchezo huu.
Kabla ya mchezo huanza, kwa kura au kwa njia nyingine, timu zinaamua ni nani atakayecheza katika shambulio hilo na ambayo mtu atakuwa katika ulinzi.
Katika siku zijazo majukumu haya yataendelea. Timu ambayo sasa inashambulia, inajaribu kupata pointi nyingi iwezekanavyo, wakati timu ya wapinzani ni kuizuia kufanya hivyo.
Lengo la timu ya kushambulia ni kama ifuatavyo: washiriki wake wanahitaji kukimbia kupitia besi zote, kisha kurudi nyumbani. Kazi ya wale wanaojitetea ni kutuma wachezaji 3 wa timu ya kupinga wasipite. Washiriki wote wa timu ya mashambulizi yanashirikiwa kwenye uwanja kulingana na mpango uliopangwa
Oky oky nisiwachanganye sana naona kama kuna watu nimewaacha kidogo lakini taratibu taratibu tutaweza kuelewa, so nataka kuwaonesha baadhi ya watu kuwa huu mchezo ni mchezo kama michezo mingine.
Nakusogezea baadhi ya wachezaji maarufu wa baseball kwa muda wote ambao ni…
- Willie Mays
Willie Mays, mchezaji bora zaidi katika historia, aliejulikana Zaidi kupitia umahiri wake katika mchezo huu ambapo alipata mafanikio makubwa, tuseme ukizungumzia timu ya taifa ya Tanzania ukitaja wachezaji wa 5 lazima umtaje Samatta, na kwa upande wa Mays ni hivyo hivyo yaani lazima umtaje tuu.
- Cy Young
Tuzo ya Cy Young ya Ligi Kuu ya Baseball imepewa jina la Cy Young, mtungi aliyeshinda zaidi kazini (511) katika historia ya mchezo huo. Bila shaka, Young alicheza katika enzi wakati wa kuanzisha viunzi mara kwa mara alipanga michezo kamili, wakati mwingine mara mbili, na wengine hata walipiga zaidi ya 300 au 400 za ndani kwa msimu.
- Grover Cleveland Alexander
Grover Alexander alikuwa wa kuvutia tangu mwanzo, akishinda michezo 28 (rekodi ya rookie), akicheza michezo 31 kamili na kukusanya innings 367 zilizopigwa katika msimu wake wa kwanza wa ligi kuu. Alikuwa mchezaji mwenye nguvu wa kulia ambaye alicheza zaidi ya michezo 40 mara nane katika msimu mmoja.
- Babe Ruth
Mtoto Ruth alizingatiwa sana mchezaji bora wa besiboli wa wakati wote kwa sababu hakuweza tu kupiga, lakini pia kurusha. Mchango wake mkubwa kwenye besiboli, hata hivyo, ni kama mchezaji wa nje. Ingawa wachezaji wawili walipita jumla ya mbio zake za nyumbani za 714.
Oooooooh! Na hao ni baadhi tu yawachezaji waliojulikana Zaidi na waliofanya makubwa kupitia mchezo huo, haya watu wangu wa nguvu msiache kufuatilia Makala zetu mbalimbali kwa ajili ya kujifunza Zaidi, www.mwananchiscoop.com.
Leave a Reply