Fahamu kuhusu homa ya nyani (monkeypox )

Fahamu Kuhusu Homa Ya Nyani (monkeypox )

Natumai niwazima wa afya wafuatiliaji wa mwananchi scoop kwenye afya tunaeleza kuhusu ugonjwa ambao unasumbua watu katika mataifa mbalimbali, hivyo basi tunatakiwa kupitia makala hii ili kuweza kuepukana nao.

Monkeypox husababishwa na virusi vya monkeypox, kirusi wa familia moja ya virusi vya ndui, ingawa sio kali sana na wataalamu wanasema uwezekano wa kuambukizwa ni mdogo. Ugonjwa huo ambao unatokea zaidi katika sehemu za nchi za Afrika ya kati na magharibi, karibu na misitu ya kitropiki.

Kuna aina mbili kuu za virusi - Afrika Magharibi na Afrika ya Kati.

Virusi hivyo viligunduliwa kwa mara ya kwanza kwa tumbili aliyefungwa na tangu 1970 kumeripotiwa milipuko ya hapa na pale katika nchi 10 za Afrika.

Mwaka wa 2003 kulitokea mlipuko nchini Marekani, mara ya kwanza ugonjwa huo kuonekana nje ya Afrika. Wagonjwa walipata ugonjwa huo kutokana na kuwasiliana kwa karibu na mbwa wa mwituni ambao walikuwa wameambukizwa na aina mbalimbali za mamalia wadogo walioingizwa nchini. Jumla ya kesi 81 ziliripotiwa, lakini hakuna iliyosababisha vifo.

Mnamo 2017, Nigeria ilikumbwa na mlipuko mkubwa zaidi kuwahi kurekodiwa, takriban miaka 40 baada ya nchi hiyo kuwa na visa vyake vya mwisho vilivyothibitishwa vya monkeypox. Kulikuwa na kesi 172 zilizoshukiwa za monkeypox, na 75% ya waathiriwa walikuwa wanaume wenye umri wa kati ya miaka 21 na 40.(source WHO)

Ugonjwa wa Monkeypox au kwa jina lingine homa ya nyani ambao umewaathiri Waafrika kwa karne nyingi, umeanza kuripotiwa katika mataifa kadhaa duniani, ikiwa ni pamoja na Marekani, Canada na mataifa kadhaa ya Ulaya.

Dalili zake

  • Dalili za awali ni pamoja na homa, kuumwa na kichwa, uvimbe, maumivu ya mgongo, kuuma kwa misuli na udhaifu wa mwili kwa ujumla.
  • Mara baada ya homa, upele unaweza kutokea, mara nyingi huanza kwenye uso, kisha kuenea kwa sehemu nyingine za mwili, kwa kawaida viganja vya mikono na nyayo za miguu.
  • Lymph nodes kuanza kuvimba ambapo kwa lugha nyingine hujulikana kama lymphadenopathy
  • Upele, ambao unaweza kuwasha sana, hubadilika na kupita hatua tofauti kabla hatimaye kutengeneza kipele, ambacho hutumbuka baadaye. Vidonda vinaweza kusababisha makovu.

Maambukizi kawaida huisha yenyewe na hudumu kati ya siku 14 na 21.

maambukizi

  • Homa ya nyani (Monkeypox) inaweza kuambukizwa wakati mtu yuko karibu na mtu aliyeambukizwa.
  • Virusi vinaweza kuingia mwilini kupitia ngozi iliyo na jeraha au michubuko, kwa njia ya upumuaji au kupitia macho, pua au mdomo.
  • Inaweza pia kuenezwa kwa kugusana na wanyama walioambukizwa kama vile nyani, panya na kindi , au kwa vitu kama vile matandiko na nguo.

Matibabu ni nini?

  • Ugonjwa huu kwanza hauna tiba maalumu (no cure), hata hivyo ugonjwa huu huisha wenyewe baada ya kumpata mtu
  • Chanjo dhidi ya ndui imethibitishwa kuwa na ufanisi wa 85% katika kuzuia monkeypox, na bado wakati mwingine hutumiwa.

Haya sasa wafuatiliaji wa mwananchiscoop uaisahu kulike na kukomenti ili uweze kupata taarifa, habari na matukio mbalimbali yanayo tokea mdani na nje ya nchi.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Detricia Pamba

A Digital Journalist, Content Creation Executive at Mwananchi Communications Ltd and Chief Editor of Mwananchi Scoop. I'm also writes stories around Technology, every Wednesday on Mwananchi Scoop. My other famous segments on Mwananchi Scoop include LISTI and WHO’S HOT.


Latest Post