Fahamu kuhusu Girlfriends Day

Fahamu kuhusu Girlfriends Day

Kila ifikapo tarehe ya leo Agosti 1, ulimwengu unaadhimisha siku ya ‘Girlfriends Day’ siku ambayo wasichana wanaopendana wanaitumia kukaa pamoja, kucheka na kushirikishana mambo yao binafsi.

Siku hii ililenga kusherekea amani na upendo baina ya marafiki wa kike na umuhimu wa kusaidiana katika maisha hata hivyo siku hii ilizidi kubamba na kuwa mashuhuri zaidi ilivyo wajumuisha wananume kwa kusheherekea na wanawake wanao wapenda.

Hafla hii kwa upande wa wanaume husherehekea na kuwaenzi wanawake bora katika maisha yao na kuwaonesha shukurani upendo kwa vitendo na hasa kuwapa maua kama njia ya kudhihirisha upendo huo.

Siku hii ni nzuri kwa kuonesha upendo na thamani ya uhusiano baina ya mwananmke na mwanaume lakini pia marafiki wa kike.

Katika yote hakikisha siku hii unaitumia katika kuandaa mlo maalumu, kutoa zawadi au kupanga shughuli ya pamoja itayomfurahisha kila mmoja pia kushiriki baadhi ya kumbukumbu nzuri au hadithi za kipekee ambazo mlipitia pamoja.

Kihistoria siku hii ilipendekezwa na marafiki wawili Allie Savarano na Sally Rodgers mwaka 2004 na kujumuishwa kwenye kalenda ya chase mwaka 2005.

Kalenda hiyo maarufu duniani iligunduliwa miaka ya 1957 na William Chase na Harrison Chase ikiwa na nia na madhumuni marejeo ya kina na yenye mamlaka yanayopatikana ulimwenguni kwa vitu maalumu iwe siku au wiki.

Kumbuka siku hii haisherehekewi kwa kupostiwa kama moja ya upendo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post