Fahamu kuhusu afya na usalama sehemu ya kazi

Fahamu kuhusu afya na usalama sehemu ya kazi

Mamboz!!! Uhali gani mfanyakazi mwenzangu nikwambie tu tumekutana tena this weekend kwenye segement yetu ya kazi kama kawaida hapa lazima nikuelekeze mambo yote yanayo husiana na kazi au vipi mwanetu.

Leo katika segment yetu ya kazi nimekusogezea ufahamu zaidi afya na usalama sehemu ya kazi.

Taratibu za kulinda usalama, afya na ustawi wa watu katika kazi au ajira kwa kuzingatia kanuni za afya na usalama mahali pake pa kazi.

Malengo ya usalama kazini na mipango ya afya ni pamoja na kuendeleza usalama na afya ya mazingira kwenye kazi yake.

Inaweza pia kulinda ushirikiano wafanyakazi, wanafamilia,waajiri, wateja na wengine wengi ambao wanaweza kuathirika na mazingira ya mahali pa kazi.

Usalama na afya sehemu ya kazi inaweza kuwa na umuhimu kwasababu ya maadili, kisheria, na kifedha.

Mashirika yote yana wajibu wa kuhudumia afya ya mfanyakazi awapo kazini ili kuhakikisha kwamba wafanyakazi na mtu mwingine yeyote ambaye haathiriki na kubaki salama wakati wote wa kazi.

Pia majukumu au sababu za kimaadili ni lazima zihusishe ulinzi wa maisha ya mfanyakazi na afya yake wakati wa kazi.

Sababu za kisheria zinazohusiana na kuzuia madhara, kwa kutoa adhabu na fidia ya sharia ya kulinda usalama wa mfanyakazi na afya yake.

Kitengo cha usalama sehemu ya kazi kitahakikisha kina punguza visababishi vya majeraha, kwakuumia na pia kwa ugonjwa kwa kugharamia huduma za matibabu, likizo ya ugonjwa na gharama ulemavu hasa kwa wafanya kazi wanao fanaya kazi hatarishi na zenye kutumia nguvu kama kazi za ujenzi.

Kitengo cha usalama sehemu ya kazi kinaweza kuhusisha mwingiliano na uhusiano kati ya maeneo mengi ya kazi, usafi wa kazi, afya ya umma, usalama uhandisi na saikolojia ya afya kazini.

Afya na usalma kazini ni jambo muhimu sana katika maendeleo ya kiwanda na kwa mfanyakazi katika ufanisi wa kazi zake, pamoja na kutambuana kudhibitihali ambayo inaweza kusababisha madhara na kuadhiri afya kutokana na kazi ambayo mtu anaifanya.

Wajibu wa mwajiri chini ya usalama na afya sehemu za kazi

@Kupima afya za wafanyakazi mara kwa mara kwa kuzingatia sheria.

@Kuchagua mwakilishi wa usalama na afya sehemu za kazi katika sehemu yenye wafanyakazi wanne na zaidi.

@Mwajiri ni lazima ahakikishe mahali pa kazi ni salama kiafya na hatakiwi kuruhusu mfanyakazi kufanya kazi yenye madhara au hatarishi kwa muda mrefu bila tahadhari.

@Ni lazima wawape wafanyakazi taarifa juu ya hatari iliyopo katika eneo la kazi na sio kuwaficha.

@Ni lazima wahakikishe hatari imedhibitiwa hadi hatua ya chini kabisa kabla ya kutoa vifaa vya kujikinga na usalama wao.

@Ni lazima watoe nguo za kujikinga pale inapolazimu kwa wale wafanya kazi za ujenzi au vibarua vigumi kiwandani.

@Ni lazima watoe mafunzo kwa wafanyakazi wanaotumia mashine na vifaa hatarishi kuhakikisha wanafahamu hatua za kiusalama itawasaidia wakiwa na elimu hiyo kwa kuwa kinga na ajali sehemu ya kazi.

@Ni lazima wawazuie wafanyakazi kutumia au kufanya kazi na vitu au mashine hatarishi mpaka kanuni zote za usalama zifuatwe.

@Ni lazima ahakikishe kwamba mashine hatarishi zinafanya kazi vizuri na ziko salama kuzitumia sio kuacha mashine mpaka zina chaka hizo zina weza kuwa hatari kubwa sana kwa waajiliwa.

@Ni lazima wahakikishe kuwa mashine hatarishi zina tahadhari au notisi kuonyesha kua ni hatari.

@Ni lazima wahakikishe kuwa mtu anyejua kazi anasimamia utendaji kazi kuhakikisha usalama wa wafanyakazi.

@Ni lazima waache sehemu za kazi wazi ili kuruhusu wafanyakazi kutoka inapotokea hatari.

Licha ya hayo mwajiri ana wajibu wa kutoa taarifa juu ya tukio au ajali yoyote iliyotokea eneo la kazi na kupelekea kifo, maumivu au majeraha ya mwili, kupoteza fahamu, magonjwa yatokanayo na kazi au yamempa ulemavu wa moja kwa moja mfanyakazi.

Ndani ya saa 24 kutoka tukio au ajali kutokea, ndani ya siku saba kutoka tukio au ajali kutolewa taarifa mwajiri anatakiwa kutuma taarifa kamili inayoelezea tukio au ajali hiyo.

Mwamba haya madini unapata wapi kama si Mwananchi Scoop nikwambie tu fupi tamu mwanetu tukutane tena next weekend.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags