Fahamu filamu iliyowahi kumfanya 50 Cent ajikondeshe

Fahamu filamu iliyowahi kumfanya 50 Cent ajikondeshe

Kawaida jambo lolote ili lifanikiwe na liwe bora linahitaji watu watakao lisimamia au kujitoa kwa nguvu zote ili kufanikisha, katika baadhi ya filamu matukio ya kila aina yamekuwa yakifanyika na watu huvaa uhusika mbalimbali.

Namna ambavyo waigizaji watauvaa uhusika katika uhalisia ndivyo itapelekea kila tukio katika filamu lionekane la kweli, watu wengi humfahamu 50 Cent kama mwanamuziki wa hip-hop, na wengina humfahamu kwa kipaji chake cha kuigiza.

Kwenye upande wa maigizo si vibaya leo kama tukijikumbushia tukio la 50 Cent la kujikondesha zaidi ya kilo 50 kwa ajili ya kuvaa uhusika kwenye filamu ya Things Fall Apart iliyoachiwa mwanzoni mwa mwaka 2011 .

Katika filamu hiyo 50 Cent aliigiza kama mchezaji wa NFL ambaye aliugua ugojwa wa saratani ambao ndiyo ulipelekea kukonda kwake, katika moja ya mahojiano yake aliwahi kueleza kuwa njia alizotumia hadi kukonda ni kutokula chakula.

Badala yake mkali huyo ambaye katika filamu hiyo alipewa jina la Deon alikuwa akinywa vimiminika maalumu vyenye lishe na kufanya mazoezi makali kwa masaa matatu kila siku  ndani ya miezi mitatu.

Hivyo basi kutokana na aina hiyo ya maisha  aliyokuwa anayafanya kwa ajili ya kuvaa uhalisia wa filamu hiyo kweli alifanikiwa na kupunguza zaidi ya kilo 50 na mwili wake ulionekana kuwa tofauti kabisa.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags