Haishangazi sana kuona nchi kubwa zaidi ulimwenguni zinaongoza kiuchumi pia kuwa na idadi ya watu wengi, mataifa kama china na India yanaongoza kwa idadi ya kuwa na watu wengi zaidi ya bilioni .
Marekani inashika nafasi ya tatu ikiwa na wakazi zaidi ya milioni 335. Nchi za BRIC (Brazil, Russia, India na China), kwa ujumla zinazochukuliwa kuwa nchi nne kuu zinazoinukia kiuchumi ambazo zinazotarajiwa kutawala ulimwengu kiuchumi kwa miaka ijayo na zote zipo katika nchi kumi za juu zilizo na watu wengi zaidi, ikionyesha umuhimu wa ukubwa wa watu wao ukiendana kabisa na ukuaji wao wa kiuchumi yaani kuna uwiano kati ya uchumi wao na wingi wa watu wao.
Kwa mujibu wa jarida la World of Statistics mataifa matano yanatajwa kuwa na utofauti mkubwa kati ya wingi wa watu na ukuaji wa uchumi wao hasa katika ukuaji wa viwanda kulingana na idadi ya watu wao.
Mataifa ambayo yapo kwenye orodha ya nchi 10 zenye watu wengi zaidi ni Urusi, Brazil, China na Marekani vilevile yanakuwa sana kiuchumi kulingana na idadi kubwa ya nguvu kazi au rasilimali watu.
Pia mataifa kama Indonesia,Nigeria,Bangladesh,Pakistan na Mexico kiuchumi hayajakuwa sana lakini yana watu wengi sana kitu kinachotajwa kuwa wingi wa watu haujaendana na ukuaji wa uchumi katika mataifa yao.
Zifahamu nchi hizo 10 zenye watu wengi zaidi duniani.
1. China 1,451,875,250
2. India 1,411,091,226
3. USA 335,407,012
4. Indonesia 280,162,730
5. Pakistan 230,953,560
6. Nigeria 218,286,375
7. Brazil 215,998,823
8. Bangladesh 168,449,149
9. Russia 146,074,197
10. Mexico 132,041,468.
Leave a Reply