Ex wako sio adui, kuna cha kujifunza hapa

Ex wako sio adui, kuna cha kujifunza hapa

Yes, moja kati ya jambo ambalo linapigwa vita katika mahusiano mengi ni pale ambapo mtu akiwa ameshindwa kuendeleza safari ya mahusiano yake na mwenza wake huwa hakuna kuachana kwa heri.

Inawezekana ukawa umeshuhudia mahusiano kadha wa kadha ambayo katika kutengana kwake hua ni vita na mwisho wa siku watu hawasemezani kabisa kutokana nayale ambayo yamesababisha wao kuachana.

Lakini je? ulishawahi kujiuliza kuwa baada ya kutengana kwa wawili hao kwa vitimbi, madhila, manyanyaso, mateso na vituko mbalimbali ambayo vimetokea kwenye safari yao ya mahusiano,kwamba kuna siku wanaweza kurudiana na kuwa pamoja?.

Hahahahaha maake  hapo kwanza ncheke, sijui kwa upande wako mdau kama unaweza kurudiana na ex wako au ndo mkishamalizana mmemalizana kila mmoja ashike njia yake.

Leo ninajambo la kuteta na nyinyi wadau kuwa kuna mengi sana ya kujifunza wakati tukiwa kwenye mahusiano na wenza wetu na pia kuachana isiwe uwadui kwani lolote linaweza kutokea na mkajikuta mmerudiana na kufunga ndoa kabisaa.

Unaamini hilo au unapingana na hoja hii? Tusiende mbali sana tujikumbushe matukio mawili makubwa ambayo kwa sasa nikikupa mifano unaweza kunielewa japo siku lazimishi Sanaa kubeba mtazamo wangu.

Hivi karibuni kulikua na tukio la Harmonize pamoja na mpenzi wake Kajala Frida kuvalishana pete katika viwanja vya Serena Hotel jijini Dar es salaam kwenye event yao ambayo ilipewa jina la HarmoJala.

Event ambayo iliyofanyika tarehe 25 juni 2022   iliyoshuhudiwa na mastar  mbalimbali akiwemo Mc Garab, Mwijaku,  mwana mitindo Martin Kandinda,Aunt Ezekiel na wengine wengi.

Baada ya kufanikisha kwa zoezi hilo ilikua faraja na furaha kubwa kwa wawili hao ambapo kupitia ukurasa wa Instagram wa Harmonize aliandika ujumbe huu


“Wen God say yes imeisha thanks for  Holding it Down Kipindi Chote Kigumu Na Kumtanguliaza Mungu Pongezi Zimekuwa Nyingi Sana ...!!! Bless up Na wanao subiri kuona tukikoseana Ni Wengi Pia Mungu Awatunze Muone Ukuu wake remember im jus traing 2b better man and my wife kajala thanks to everbody did this” Aandika Harmonize

Licha ya changamoto mbalimbali ambazo walipitia wawili hawa na kufikia hatua ya kila mmoja kufanya maisha yake lakini leo hii tunazungumza mengine kuhusu wawili hao.

Tujikumbushe machache kabla ya penzi hilo kurudi tena mjini, ambapo Juni 5 mwaka huu kutoka ukurasa wa harmoni aliandika ujumbe akiwa anamuomba  radhi mchumba wake huyo

“This is not Apologise Post ..!!!! Its Appreciation Post To Someone that I was almost to lose  wakati dunia nzima inasema haiwezekani ulisimama ukasema inawezekana you loved me mbaya zaidi ulikutana na disappointment ambayo ilimpa nguvu na ujasili wa kila mtu aliekaribu yako kusema mimi sio bina damu wakuwa hata karibu yako

“ I'm sure uliumia sanaa ...!!!! still hukunikatia tamaa wakati mwingine binadamu huingia kwenye mahusiano ukiamini kwamba unaweza msahau yule uliekuwa nae mwanzo bila kuwaza niini kiliwafanya muwe pamoja”

“Nilipitia hicho kipindi na picha zika mwagika mtandaoni na nikajiona nimemaliza wala sikujali maumivu yako still ulikaa kimya no interview richa ya kuahidiwa marundo ya pesa ambayo ungeweza nunua hata hivyo vigari wanavyo viona ni kitu cha maana sana “

Alooooh!! Ukiachana na couple hiyo bwana  siku chache zilizopita ambapo Mastaa wa kubwa hapa nchini wa muziki wa bongo fleva Nandy pamoja na mume wake Billnas nao walifanikisha jambo lao la kufunga ndoa.

Ikumbukwe kuwa wawili hao hadi kufikia hatua hiyo yako mambo mengi sana ambayo wamepitia ikiwemo suala la kutengana kwao, lakini leo hii tunazungumze mengine.

Billnas pamoja na Nandy walifunga ndoa, Jumamosi, 16/07/2022 katika kanisa la kiLutheri, Mbezi beach  na sherehe kufanyika katika ukumbi wa Mlimani City.

Ndoa yao ilihudhuriwa na mastaa kibao. Maharusi hao walipatiwa zawadi ya zaidi ya milioni 200 na gari juu. Huu ni mfano hai wa alipangalo Mungu, mwanadamu hawezi kulitenganisha.

Kwenye mahusiaono tunatakiwa kujifunza kuwa mpenzi wako ulieachana naye isiwesababu ya vita na uhasama baina yenu kwani wakati mwingine mnatengana na kupeana muda ili kila mmoja akapambinie kombe kwingine akisoma alama za nyakati.

Hata hivyo mkiwa mmpetia mapito mengi basi utagundua jambo tu na pia ukawa mwanzo mzuri wa kurejeana na kuendeleza maisha yenu hahahaha alooooo tukumbuke kauli hii 'Ex wako sio adui yako'. acha dharau, kauli chafu na kejeli kwa mtu ulieachana nae.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags