Mamlaka ya Vyombo vya Habari vya Ethiopia (EMA) ambayo iko chini ya Serikali imetoa onyo kwa mamlaka nyingine ambazo zimekuwa zikiingilia Uhuru wa Waandishi wa Habari wakiwemo wanaofanya Habari za uchunguzi.
Onyo hilo limetokana na malalamiko ya Kituo cha Runinga cha EsatTv kudai imepokea barua ya Vitisho kutoka Mahakama ya Addisababa ikiwataka Waandishi wake kuachana na Habari za Uchunguzi
Kwa mujibu wa Taasisi ya “reporters without borders” (RWB) uhuru wa maoni na vyombo vya Habari chini ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed bado una mgawanyiko ingawa kuna Mabadiliko makubwa kulinganisha na Utawala uliopita. Na zaidi ya Vyombo vya Habari 200 vilivyopigwa marufuku Vimefunguliwa.
Leave a Reply