Esma Platnumz asema hababishiwi na wanaume

Esma Platnumz asema hababishiwi na wanaume

Aloooh dada wa msanii Diamond, Esma Platnumz  amefunguka kuwa haoni sababu ya kuteswa kwenye mapenzi/mahusiano wakati ana uwezo wa kusimamia mambo yake yote na sio kisa ni dada wa Diamond bali yeye binafasi ana uwezo wa kusimamia mambo yake, hivyo haoni sababu ya kukaa anaumia kwenye mahusiano na wakati anaweza kutafuta pesa mwenyewe.

Esma ameshare ujumbe huo kupitia ukurasa wa wake wa Instagram huku akisisitiza kuwa yeye ana uwezo wa kusimamia mambo yake.

"Sijimwambafai kwasababu ni dada yake flani, mimi najiamini na najikubali kwasababu ni mwanamke ambaye natafuta mwenyewe, najua kutafuta pesa, najua kulipa kodi, najua kujijengea, najua kulisha watoto wangu, nina wafanyakazi nyumbani, nina walinzi ninasomesha watoto wangu, nina kila kitu kinachojitosheleza.'' 

''Kwahiyo mwanaume hawezi nibabaisha, nikiona hatuelewani namwambia ashike na mimi nishike huku yanini nipate stress ndugu yangu maisha yenyewe mafupi nishateswa huko saana hata huu utu uzima wangu nianze kuteseka na mapenzi? hapana kwakweli siwezi.'' 

Ebwana eeeh!! Dondosha maoni yako kupitia ujumbe huo aliouachia bibie Esma Platnumz.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags