Eric Omondi akamatwa tena na polisi

Eric Omondi akamatwa tena na polisi


Mchekeshaji Eric Omondi amekamatwa tena na polisi nchini Kenya, wakati alipokuwa kwenye maandamano yanayoendelea nchini humo ya kupinga ongezeko la kodi katika Muswada wa Fedha wa 2024/ 2025.

Kupitia video ambazo zimesambaa mitandaoni zinamuonesha mchekeshaji huyo akikamatwa kinguvu na polisi huku akisikika sauti yake ikisema “Kama ndugu yangu aliuliwa na mimi mje muniue”.

Ikumbukwe kuwa siku sita zilizopita kaka wa mchekeshaji huyo aitwaye Fred Omondi alifariki dunia baada ya kupata ajali ya kugongwa na gari jijini Nairobi.

Hii si mara ya kwanza kwa mcheshi huyo kukamatwa, mwanzoni mwa mwezi huu alikamatwa kwa kuongoza maandamano nje ya Jengo la Bunge, pia Mwezi Februari mwaka jana, alikamatwa kwa kuongoza maandamano dhidi ya gharama kubwa ya maisha ambayo pia aliyafanyia nje ya Majengo ya Bunge.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post