Erdogan aapa kuijenga Uturuki upya

Erdogan aapa kuijenga Uturuki upya

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ameapa kuijenga nchi hiyo upya kufuatiwa na tetemeko la ardhi  lililotokea usiku wa kuamkia February 6 ambalo limeleta uharibifu mkubwa wa majengo na mali.

Jumla ya vifo mpaka sasa nchini Uturuki na Syria imefikia zaidi ya watu 41,000, na manusura wengi wanakabiliwa na baridi kali baada ya kuachwa bila makazi kutokana na uharibifu mkubwa uliofanyika katika miji ya nchi hizo mbili.

Erdogan amesema wataendelea na kazi hadi watakapomuondoa raia wa mwisho aliyebaki kwenye majengo yaliyoporomoka, amesema tathmini ya majengo ambayo maelfu yaliharibiwa itakamilika katika wiki moja na ujenzi mpya kuanza katika miezi kadhaa






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags