Epuka kula vyakula hivi usiku

Epuka kula vyakula hivi usiku

Watu wengi wamekuwa wakifikiria kuwa unene ni fahari, heshima lakini wanasahau au hawajui kuwa yapo madhara mengi ambayo yanajificha nyuma yake.

Imekuwa ikidhaniwa kuwa mtu kuwa mnene ni kufanikiwa kiuchumi na katika maisha yao, lakini uchunguzi wa kitaalamu unaonesha kuwa watu wanene wapo katika hatari ya kupata maradhi yasiyoambukiza kama kisukari, ugonjwa wa moyo pamoja na kiharusi.

Inaelezwa kuwa matumizi ya baadhi ya vyakula na kutokujua vyakula gani wale na kwa wakati gani bado ni tatizo kwao.

Kwa kulitambua hilo, leo wataalaamu wanaeleza vyakula ambavyo havipaswi kuliwa usiku na kama ukivila ni athari gani za kiafya utaweza kuzipata.

Moja ya athari kubwa zaidi kama utakula vyakula hivyo ni kuongezeka uzito bila mpangilio, kukosa usingizi na kulala kama mfu kutokana na tumbo kujaa au kulala usingizi wenye kukatika katika.

Wataalamu wa afya wanashauri kwamba ili kuepuka na athari hizo ni vyema watu wanene wakatumia matunda, mbogamboga au vyakula vingine ambavyo vina kalori na mafuta kidogo au visiwe na mafuta kabisa.

Baadhi ya vyakula ambavyo ni marufuku mtu kula usiku

Moja, Vyakula vilivyoandaliwa na mafuta mengi

Hii ni aina ya vyakula ambavyo mtu hupaswi kula usiku kwa sababu havikufanyi ujisikie uchovu na uvivu asubuhi ya siku inayofuatia bali pia humpa msukosuko mtumiaji wa kwenda kujisaidia mara kwa mara.

Vyakula vyenye wanga kwa wingi au vyenye sukari kupitiliza

Kundi hili ndilo watu wengi hulichanganya kwa kuamini tambi ni chakula chepesi kuliwa usiku, kitu ambacho si sahihi.

Tambi ni moja ya vyakula ambavyo havipaswi kuliwa usiku kwani ina wanga mwingi ambao kutokana na kulala hakisagiki na kinaweza kuziba mirija ya damu na kusababisha madhara kwa mtumiaji.

Pia ice cream nayo hupaswi kula usiku kwa kuwa ina sukari na uongeza uzito bila sababu.

Nyama nyekundi na vyakula vyenye protini nyingi

Kula nyama nyekundu usiku kunamfanya mhusika asipate usingizi mzuri kwa kuwa tumbo linashindwa kusaga vyakula vigumu uwapo usingizini.

Kama ni lazima kula nyama basi ni vyema ikawa nyeupee kama vile kuku na samaki, pia ni muhimu kuepuka vyakula vyenye protini. Ikishindikana basi glasi ya maziwa ya mtoto inaweza kukidhi haja bila kuwa na madhara.

Kahama

Kwa kawaida, kahawa ina kafeini ambayo inaweza kusababisha usumbufu wakati wa kulala kwani hata dawa zenye kafaeini hapaswi kupewa mgonjwa wenye matatizo ya kupata usingizi.

Vivyo hivyo kwa asiyekuwa mgonjwa ina madhara pia hap ahata soda ambazo zina kafeini pia si nzuri kwani zinasababisha mtumiaji kukosa usingizi wa kutosha na kushndwa kufanya mambo yake kwa mpangilio maalum unaofaa.

Hizo ni baadhi ya vyakula tumekuwekea leo unaweza kuamua kuanzia sasa kuachana na vyakula hivyo nyakati za usiku na utakuja kuniambia matokeo yake.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post