Elon Musk arudi kuwa tajiri namba moja duniani

Elon Musk arudi kuwa tajiri namba moja duniani

Boss wa Makampuni ya SpaceX, Tesla na Twitter, Elon Musk amerudi tena kuwa Tajiri namba moja Duniani baada ya kuondolewa kwenye nafasi hiyo mwishoni mwa mwaka jana baada ya kutumia USD Bilionea 44 kuinunua Twitter.

Jarida la Bloomberg limesema ukuaji wa thamani za hisa za kampuni ya magari ya umeme ya Tesla umeinua utajiri wa Musk hadi kufikia thamani ya USD Bilioni 187.1 kufikia mwanzoni mwa wiki hii baada ya soko la hisa kufungwa, ikifuatiwa na utajiri wenye thamani ya USD Bilioni 185.3 wa Arnault.

Ikumbukwe mwishoni mwa mwaka jana Mkurugenzi Mtendaji wa Elon Musk alitolewa kwenye nafasi ya kwanza kwenye orodha ya Matajiri zaidi duniani na kiti hicho kilikaliwa na Bernard Arnault, Mkurugenzi Mtendaji wa chapa ya kifahari kutokea nchini Ufaransa LVMH (ambaye ni Mmiliki wa chapa za Hennessy, Moet Chandon Louis Vuitton n.k) na kumfanya Musk ashike nafasi ya pili kwa zaidi ya miezi miwili.

Aidha hivi karibuni Elon Musk aliweka wazi kuwa tayari ameonesha nia ya kuwekeza Tanzania kupitia Star Link ambapo Waziri wa Habari, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Nape Nnauye amesema Serikali ya Tanzania imeshatoa majibu kwa kampuni ya Starlink na vikao vinaendelea ili wakamilishe documents na waruhusiwe kuanza huduma zao Tanzania.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post