Elon Musk ahudhuria harusi ya Ex wake

Elon Musk ahudhuria harusi ya Ex wake

Mmiliki wa mtandao wa X (zamani Twitter) na mfanyabiashara Elon Musk ameripotiwa kuwa na maelewano mazuri na aliyekuwa mke wake Talulah Riley hii ni baada ya kuonekana kwenye harusi ya mwanadada huyo.

Kwa mujibu wa tovuti ‘The Time’ imeeleza kuwa bilionea huyo alifika katika harusi hiyo iliyofanyika nchini Ungereza, katika mji wa Anstey akitokea Ufaransa ambapo aliweza kushuhudia maharusi hao wakila kiapo.

Uwepo wa bilionea huyo mwenye umri wa miaka 52, katika harusi unaonesha jinsi alivyo karibu na Talulah mwenye umri wa miaka 38, ingawa wameachana miaka kumi iliyopita.

Utakumbuka Talulah na Elon walichumbiana mwaka 2008, na kufunga ndoa mwaka wa 2010 katika Kanisa Kuu la Dornoch huko Scotland mwaka 2016 waliachana.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags