Eddie Ngwasuma kazi ya sanaa haihitaji hasira

Eddie Ngwasuma kazi ya sanaa haihitaji hasira

It’s blue Monday wadau wameamua kuipa jina hilo bwana, ndani ya Mwananchi Scoop kila ifikapo siku hii huwa kwetu tunazungumzia masuala mazima ya kazi, ajira na maarifa mbalimbali ili kuhakikisha tunakupa mawazo chanya katika utafutaji wako wa kila siku.

Nikwambie tu leo kwenye makala ya kazi namleta kwako Edward Mbogo maarufu kama Eddie Ngwasuma kijana ambaye anajihusisha na kazi ya Uigizaji wa series mbalimbali hapa nchini.

Ngwasuma anasema kuwa yeye Uigizaji kwake ni Kazi ambayo anaikubali na kuiheshimu sana, tofauti na watu wengine wanavyoichukulia katika jamii.

Akizungumza na Mwananchi Scoop Ngwasuma alisema kuwa kazi hiyo inahitaji mtu kuifanya kwa moyo na umakini mkubwa ili kuepuka kuipotosha jamii.

Aidha alisema kuwa kazi hiyo inahitaji mtu kuwa karibu na jamii, kujua changamoto na maisha kwenye jamii kwani unapofanya kazi hiyo, unatakiwa kusimama kwa ajili ya kuisemea jamii kupitia mambo mbalimbali.

Vile vile alisema ni kazi ambayo inahitaji ushirikiano wa hali ya juu, na mtu anatakiwa kuwa makini mnoo katika kila jambo ambalo analifanya ili kuhakikisha anafanya kwa kuzingatia maadili bila kuipotosha jamii.

Sambamba na hayo alielezea ugumu wa kazi hiyo na kubainisha kuwa jamii huwa na mitazamo tofauti pale ambapo mtu anapovaa uhusika ambao ni tofauti na jinsia aliyonayo.

“Unapewa character ambayo kwenye jamii unaipinga mfano unaweza kuvaa uhusika wa mtu ambaye anashiriki mapenzi ya jinsia moja ni kazi ndiyo umepewa na unalipwa vizuri lakini jamii inakuchukuliaje baada ya hiyo kazi” alisema na kuongeza

“Ukizingatia unafamilia, unawazazi, mke, watoto na ndugu wengine hivyo huwa kunachangamoto nyingi pale unapopata character za aina hii” alisema

Hata hivyo alisema changamoto nyingine jamii imechelewa kupata uelewa juu ya kazi za sanaa kwani awali watu walikuwa wanachukulia kama vile ni masuala ya kihuni.

Vilevile alisema kuwa ili kuhakikisha unafanya kazi yako vizuri, inakubidi uwe mtu wa kufuatilia mambo yanayoendelea katika jamii na duniani kwa ujumla kwani mambo yanabadilika.

“Uwe mwepesi kujiupdate Kama hubadiliki mapokeo yako hayawezi kuwa chanya kwani mambo yanabadilika, uwe flexible watu wanaichukulia nyepesi lakini ni kazi ambayo inahitaji muda wa kutosha wa kufuatilia vitu na kusoma pia”alisema.

Akizungumzia Changamoto kubwa katika kazi hiyo amesema kuwa baadhi ya watu ambao wanawafanyia kazi sio waaminifu hususani katika masuala ya mikataba.

Pia alisema kuwa wako watu ambao hawapo serious kabisa katika kile ambacho unakifanya, na jamii bado haijaichukulia serious kazi hiyo.

‘Kwa sisi wanaume ambao inafika wakati unahitaji kuoa basi unakuta unakwenda kuposa wakishakujua tu unajihusisha na masuala ya sanaa inakua tatizo kuaminika kwani bado unaonekana hauko serious na maisha”alisema

Hata hivyo aliwataka vijana ambao wanatamani kufanya kazi hiyo kuhakikisha wanajichunguza kabla hawajaingia kwenye kazi hiyo, nakuwataka kukubali kukosolewa na wasiwe watu wa hasira kwani kazi hiyo inahitaji sana mabadiliko.

Aidha alisema kuwa ili kazi hiyo iweze kufika mbali zaidi Serikali inatakiwa kuweka nguvu, kwani kupitia sanaa kuna mapato mengi ambayo yanapatikana.

“Sera ziboreshwe, sera zibadilishwe mapato mengi ya kazi za sanaa yanapotea kiujanja ujanja kwa wizi mitaani, kwani pesa ambayo mtu anaiwekeza huwa hairudi kama vile alivyo tarajia”alisema.

Vilevile akielezea mtindo wa series ambao Kwa sasa takribani media mbalimbali wanautumia, alisema kuwa ni mzuri kwani umeweza kubadilisha wanatasnia hasa katika maslahi yao.

Aidha alisema kuwa mtindo huo kwa sasa unalipa tofauti na hapo awali, nakuzitaka media nyingine ziweze kuwekeza katika mtindo huo.

Hata hivyo alisema kuwa kwa sasa jamii inauelewa mkubwa juu ya mtindo huo wa series tofauti na mtindo wa Cd ambao ulikua ukishamiri hapo awali.

“Mtindo wa series unatusaidia sana sisi kwani unatufanya tunakuwa bize na kazi, ukichukulia mfano wa movie unaweza ukatumia miezi miwili kufanya then ukakaa hata miezi sita bila kazi lakini kwenye series ni tofauti sana kwani ni project ambayo inamuendelezo” alisema.

Vilevile alisema wasanii ambao wanafanya mtindo wa series wanatakiwa kutambua kuwa mtindo huo unafuatiliwa sana na watu  na wanajifunza, hivyo wanapopata nafasi ya kufanya kazi waonyeshe uwezo walionao.

Pia alisema wanatakiwa kutambua kuwa jamii inawafuatilia na wanajifunza kupitia wao, hivyo wafanye vitu kulingana na maadili husika.

Hata hivyo alisema malengo yake ni kuhakikisha anawekeza katika upande mwingine ili kuacha kutegemea katika sanaa moja kwa moja.

Sambamba na hayo alitaja  kipaumbele chake katika  maisha yake ya kila siku ikiwa ni kuwa flexible ili asitoke kwenye ramani katika kazi ambazo anazifanya.

Je kitu gani ukifanyiwa ni mwepesi Sana kupanic?

“Mtu kunisababishia fedheha, sipendi kufedheheshwa afanye jambo ambalo litashusha hadhi yangu katika jamii na kusababisha nidharaulike hilo suala mimi sikubaliani nalo”alisema.

Kabla ya kujihusisha na Kazi ya Sanaa awali ulikua unafanya Shughuli gani?!

“Kabla sijajihusisha na sanaa mimi by professional ni sociologist nimeshafanya kazi katika makampuni binafsi ya usafirishaji lakini sanaa imekua na nguvu zaidi kuliko kitu mbacho nimekiendea darasani”alisema.






Comments 1


  • Awesome Image
    Chris BANDA 1st Edition

    Man you made me proud for what your doing keep it up ur doing great

Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags