Drogba akanusha kubadili dini

Drogba akanusha kubadili dini

Mchezaji maarufu wa zamani kutoka Ivory Coast, Didier Drogba amekanusha madai kwamba amebadilisha dini yake na kuwa Muislamu na kuongeza kuwa alishangazwa na jinsi taarifa hiyo ilivyosambaa.

Taarifa hiyo ilisambaa baada ya kiongozi mmoja wa Kiislamu anayefahamika kwa jina Dr. Mohamed Salah anayeishi Marekani kuchapisha picha inayoonyesha Drogba akisali kama Waislamu na kusema kwamba Drogba ameslim na hivyo ndivyo taarifa hiyo ilivyoenea kupitia mitandao ya kijamii.

Saa chache baadaye, Drogba alituma ujumbe kwenye mtandao wake rasmi wa Twitter akikanusha madai kwamba alibadilisha dini.

"Nilikuwa ninatoa heshima kwa kaka zangu Waislamu niliokuwa nimewatembelea. Lilikuwa ni tukio ambapo tulionyesha umoja lakini sijabadili dini," ameandika Drogba katika ukurasa wake wa Twitter.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post