Dream Doll atumbuiza wimbo wa Rayvanny Uingereza

Dream Doll atumbuiza wimbo wa Rayvanny Uingereza

Rapa kutoka nchini Marekani Dream Doll ametumbuiza wimbo wa mwanamuziki wa Bongo Fleva Rayvanny uitwao ‘Shake shake’ nchini Uingereza alipokuwa katika zira yake.

Kupitia Insta story ya mwanamuziki huyo mwenye umri wa mika 32 amechapisha video akiwa anatumbuza wimbo huo Jijini Londoni.

Utakumbuka wimbo wa ‘shake shake’ ulitoka Mei mwaka jana ambapo Doll alishirikishwa na msanii huyo baadhi ya mistari na mpaka sasa unawatazamaji Milioni 1.

Dream Doll amewahi kufanya wimbo kama, Different, Watchu like, Who you loving, Ice cream dream, Everthings Nice, You know my Body na nyingine nyingi.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post