Drake azishitaki UMG, Spotify kisa Not Like Us ya Kendrick

Drake azishitaki UMG, Spotify kisa Not Like Us ya Kendrick

Rapa Drake ameripotiwa kuishitaki mitandao ya kuuzia muziki Universal Music Group (UMG) na Spotify kufuatia na wimbo wa Kendrick Lamar.

Kwa mujibu wa Billboard, Drake amechukua hatua za kisheria dhidi ya mitandao hiyo kwa madai kuwa kampuni hizo mbili zilifanya kazi pamoja ili kuongeza ushawishi kwenye wimbo huo wa Lamar.

Drake ametoa malalamiko hayo jana Jumatatu Novemba 25 katika mahakama ya Manhattan ambapo kampuni ya Drake Frozen Moments LLC, inashutumu UMG kwa kutumia mbinu haramu kama vile Bots, Payola, na mbinu zingine za kuongeza streams bandia kwenye wimbo wa Not Like Us.

Aidha UMG imeshitakiwa kwa kutekeleza mipango ya kudhibiti mifumo ya streams na redio badala ya kufuata utaratibu wa kawaida wa mitandao hiyo.

Mawakili wa Drake wanasema kuwa vitendo hivi vilikiuka Sheria ya shirikisho ya RICO, sheria inayotumika katika kesi za uhalifu uliopangwa, pamoja na sheria za jimbo la New York kuhusu vitendo vya udanganyifu vya biashara na matangazo ya uwongo.

‘Not Like Us’ ya Kendrick ilitoka May 5, 2024 ikiwa ni muendelezo wa disstrack walizo kwa kwakitupiana kati ya rapa hao ikiwa ni miongoni mwa nyimbo zilizompa mafanikio mkubwa Kendrick ambapo inazaidi ya watazamaji million 178 kwenye mtandao wa YouTube huku ikichaguliwa kuwania tuzo za Grammy 2025 kwenye vipengele 5.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags