Drake aendelea alipoishia

Drake aendelea alipoishia

Imekuwa desturi kwa mwanamuziki kutoka Canada, Drake kutoa maokoto kwa mashabiki wake kama zawadi, sasa amemzawadia shabiki yake ambaye ni mjamzito dola 25,000 sawa na tsh 63.5 milioni.

Drake alitoa pesa hizo akiwa katika show yake weekend baada ya shabiki huyo kuinua bango lililokuwa limeandikwa ‘Nina ujauzito wa miezi mitano unaweza kuwa baba tajiri wa mtoto wangu’ ndipo msanii huyo akasimamisha show kwa muda na kumpatia kiasi hicho cha pesa ili aweze kuwa baby mama tajiri.

Huu unakuwa muendelezo kwa Drake kuwawezesha mashabiki, ikumbukwe kuwa Machi 3 mwaka huu akiwa kwenye ziara yake ya ‘it’s All a Blur’ jijini Kansas alimlipia shabiki yake mkopo wa nyumba uliokuwa ukigharimu kiasi cha dola 160k ambayo ni sawa na tsh 408 milioni.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags