Dj Spinall awakutanisha Tyla na Omah Lay

Dj Spinall awakutanisha Tyla na Omah Lay

Wakitajwa watu ambao wamehusika kwa kiasi kikubwa kuupeleka kimataifa muziki wa Nigeria ni ngumu kuacha kumtaja Dj maarufu nchini humo Oluseye Desmond Sodamola au DJ Spinnal.

Spinnal ambaye anaweza kuwa amejishinda mwenyewe kwenye wimbo wake mpya uitwao "One Call," baada ya kuwashirikisha Omah Lay na Tyla ambao ni vijana wanaokimbiza kwenye soko la muziki wa Afrobeat Duniani.

Wimbo huo mpya unaonesha uwezo wake wa kuunganisha wasanii wawili ambao wanaimba muziki wa aina tofauti tofauti na kuweza kupata kitu kimoja kwani wasanii hawa wawili wanatokea nchi mbili tofauti ambazo kila moja ina aina yake ya muziki.

Hivi majuzi, Spinnal alikua DJ wa kwanza kutokea Barani Afrika kutumbuiza kwenye tamasha kubwa linalofahamika kama Coachella, ambalo kwa mwaka huu lilifanyika California nchini Marekani, Mbali na Kolabo hiyo mpya pia Spinnal ameshafanya kazi na wasanii maarufu na wakubwa kama vile Wizkid, Tiwa Savage, Burna Boy, na Davido.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags