Ditopile awashukia waliombeza Rais Samia kuhusu uendelezaji wa miradi ya kimkakati

Ditopile awashukia waliombeza Rais Samia kuhusu uendelezaji wa miradi ya kimkakati

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma, Mariam Ditopile amesema Rais Samia Suluhu Hassan ndani ya muda mfupi madarakani anazidi kuwaumbua wale wote waliombeza kuhusu uendelezaji wa miradi ya kimkakati Jiji la Dodoma iliyo asisiwa na Mtangulizi wake Hayati Dk. John Magufuli.

Mbunge Ditopile ameyasema hayo leo Februari 9, 2022 katika hafla ya Rais Samia ya kuweka jiwe la msingi barabara ya mzunguuko wa nje ya Jiji la Dodoma yenye urefu wa km 112.3. Barabara hiyo itatoka Ihumwa-Matumbulu-Nala-Veyula-Ihumwa.

Amesema anampongeza Rais Samia kwa kuendelea kutimiza ahadi zake kwa vitendo hasa kuendeleza miradi yote ya kimkakati iliyoasisiwa na Hayati Dk. Magufuli Jijini Dodoma kwa kasi kubwa.

"Yalikuwepo maneno kwamba Hayati ameondoka na miradi itasimama au haitafanyika lakini sasa ni tofauti, miradi yote inaendelezwa. Mradi huu wa ujenzi wa barabara ya mzunguko wa nje wa Jiji la Dodoma ni mradi ulisubiriwa kwa hamu na wana Dodoma utalibadilisha hili jiji letu.

"Mradi mwingine unaendelezwa na Rais Samia Jijini Dodoma ni ujenzi wa hospitali mpya ya Jiji la Dodoma na tayari Rais ametoa zaidi ya Milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wake kuanza, sisi wana Dodoma tunamshukuru na kumpongeza Sana" amesema

Aidha amesema Rais Samia anaonyesha kwa vitendo anayo nia ya dhati ya kuendeleza miradi yote ya mtangulizi wake, hivyo anawasihi watanzania kupuuzia maneno ya watu wachache wasioitakia mema nchi yetu na kusisitiza kuwa  Rais atatekeleza miradi yote aliachiwa tena kwa kasi kubwa na ufanisi.

"Hii miradi mfano njia mchepuo Kusini Jiji la Arusha 42.4Km, Barabara ya Mbinga-Mbamba Bay 66 Km, Barabara ya Singida-Babati-Minjingu 223.5Km, Barabara ya Arusha-Namanga 105Km, Iringa- Dodoma 260Km, Namtumbo-Tunduru 190Km, Mayamaya-Bonga 188Km, Tunduru - Mangaka Mtambaswala 202.5KM yote inaendelea kutekelezwa na itakamilika kwa wakati, huyu ndo Rais Samia wa vitendo sio maneno" amesema






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags