Director Khalfani kuzikwa leo saa 10 jioni

Director Khalfani kuzikwa leo saa 10 jioni

Maziko ya muongozaji wa video za muziki nchini Tanzania na filamu maarufu Director Khalfani Khalmandro yatafanyika leo saa 10 alasiri katika Makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Mwanaspoti mdau wa muziki na Meneja wa msanii Diamond Platnumz, Said fella (Mkubwa Fella) amesema “taratibu za maziko zinafanyika na tutampumzisha mpendwa wetu saa 10:00 Jioni makaburi ya Kisutu”.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kutoka Taasisi ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu Muhimbili (MOI), Patriki Mvungi, Khalmandro amefariki wakati akiendelea kupatiwa matibabu katika taasisi hiyo.

Taarifa za awali zilieleza kuwa Director Khalfan alifikishwa Hospitali ya Taifa Muhimbili akiwa na tatizo la damu kuvilia kwenye ubongo, lililosababisha changamoto ya kupooza upande wa kulia wa mwili wake.

Enzi za uhai wake Director Khalfani alikuwa miongoni mwa watengenezaji video bora nchini na alifanya kazi na wasanii mbalimbali akiwemo Ben Pol, Christian Bella, Madee, Aslay, Shilole, Nuh Mziwnda, Maua Sama, Navykenzo, Baby Madaha, Chinbees, Bob Junior, Linah Sanga, Q Chilla, na wengine wengi.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags