Director khalfani afariki dunia

Director khalfani afariki dunia

Aliyekuwa muongozaji wa video za muziki nchini Tanzania, Director Khalfan Khalmandro amefariki dunia alfajiri ya leo Mei 5, 2024 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.

Taarifa zilieleza kuwa Khalfan alilazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, taasisi ya mifupa MOI akiwa na tatizo la damu kuvilia kwenye ubongo lililopelekea changamoto ya kupooza upande wake wa kulia wa mwili.

Enzi za uhai wake alishawahi kufanya video za wasanii kama Ben Paul katika wimbo wa ‘Nyumbani’, Linah, Marioo katika wimbo wa ‘Yesa’, Stamina katika wimbo wa ‘Machozi’, Q chief katika wimbo wa ‘Babyoo’ ‘, Weusi katia wimbo wa ‘Bado hauja balrhe’ , Madee Ali katika wimbo wa ‘Pazuri’ na wengine wengi.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags