Baada ya record lebo ya ‘Pozi Kwa Pozi’ (PKP) iliyokuwa chini ya msanii wa Bongo Fleva, Ommy Dimpoz kufanya vizuri miaka ya 2016 ikiwa na msanii wake Nedy Music, hatimaye Ommy Dimoz ametangaza kuifufua tena Lebo hiyo ambayo ipo kimya kwa muda mrefu.
Akizungumza na Mwanachi Scoop Jana Jumatatu, Februari 17, 2025 Dimpoz ameweka wazi kuwa mipango yake ni kuwekeza hela nyingi kwenye lebo hiyo ili kuwe na mafanikio makubwa kwa wasanii watakao sainiwa chini yake.
“Ndio maana mimi huwa nasema watu wananiuliza unafungua lini lebo nawambia kwamba nataka kujipanga ili siku nikimtambulisha msanii yaani nimerudi sasa na PKP iwe kweli kwenye hatua nzuri na hela ya maana niwekeze, bila shaka mpango wa kurudi ninao" Amesema Dimpoz.
Kutokana na ingia toka za wasanii kwenye lebo za muziki nchini kwa upande wake Dimpoz haimtishi kwani hali hiyo ni ya kawaida kwa wasanii kukubwa.
“Hapana yaani unaona hata wenzetu hii industry ni kubwa kwaiyo hiyo lazima iwepo sana sana ntaomba ushauri kwa wamiliki wakubwa wa lebo za Muziki kwa sababu wanasema muige yule aliye fanikiwa au omba ushauri kwa walio fanikiwa ndio watakushauri vizuri,”amesema Dimpoz.
Record lebo ya PKP ilifanikiwa kumsimamia msanii Nedy Music ambaye alitoa nyimbo nyingi ikiwa ni pamoja na Usiende Mbali, Nshalewa Ft Mr. Blue, Rudi ft Christian Bella na nyingine nyingi.

Leave a Reply