Diddy na tuhuma za ukatili wa kingono

Diddy na tuhuma za ukatili wa kingono

Mwanamuziki na muigizaji maarufu kutoka nchini #Marekani #Cassie amemtuhumu mkali wa Hip-Hop #Diddy kuwa aliwahi kumfanyia ukatili wa kingono kwa zaidi ya miaka 10 walipokuwa na uhusiano wa kimapenzi.

Cassie amedai kuwa #Diddy aliwahi kumbaka na kumuhusisha na biashara za kingono. Aidha aliendelea kwa kueleza baada ya kusainiwa katika ‘Lebo’ ya ‘Bad Boy Records’ inayomilikiwa na #Diddy, #Cassie akiwa na umri wa miaka 19, aliingizwa katika matumizi ya vilevi vikali na Dawa za Kulevya jambo lililochangia kuathiri maisha yake binafsi na kimuziki.

Kutokana na tuhuma hizo Mwanasheria wa #Diddy, amezikanusha na kueleza kuwa #Cassie alitaka kulipwa dola milioni 30 ili aweze kukaa kimya, huku upande wa mwanadada huyo alidai kuwa #Diddy ndiye aliyetaka kutoa fedha ili kumnyamazisha kwa sababu anataka kuwasaidia Wanawake wanaopitia ukatili katika mapenzi.

Hii siyo mara ya kwanza kwa #Diddy kukutana na tuhuma nzito kwa mwaka huu, mwezi mmoja uliyopita, mtuhumiwa namba moja wa mauaji ya #Tupac, Davis Keefe D alidai kuwa alilipwa dola bilioni 1 na #Diddy ili kutekeleza mauaji ya Tupac yaliyotokea mwaka 1996.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags