Diddy aonekana akila bata na mabinti zake

Diddy aonekana akila bata na mabinti zake

DIDDY AONEKANA AKILA BATA NA MABINTI ZAKE

Baada ya kushutumiwa na kufunguliwa mashitaka dhidi ya kesi za unyanyasaji wa kingono huku kutojulikana alipo na sasa mwanamuziki Diddy ameripotiwa kuonekana akila bata na watoto wake wawili Jessie na D’Lila ambao ni mapacha.

Diddy ameonekana akiwa na watoto wake hao jijini Miami katika sehemu ya kucheza Golf ambapo kunadaiwa kuwa ni mtaa ule ule ambao polisi walifanya msako wa nyumba yake.

Diddy anaweza kuwa huru uraiani kwa muda usio julikana kutokana na polisi kutokuwa na ushahidi wa kutosha kumtia nguvuni , huku upelelezi ukiendelea ambapo unasubiriwa wakati wa Diddy kuitwa mahakamani kwa ajili ya kujibu tuhuma hizo za kujihusisha na biashara za ngono.

.
.
#mwananchiscoop
#burudikanasi


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post