Diddy agonga mwamba, mahakama yatupilia mbali rufaa ya kuomba tena dhamana

Diddy agonga mwamba, mahakama yatupilia mbali rufaa ya kuomba tena dhamana

Mwanzoni mwa wiki hii, Diddy alikamatwa kufuatia miezi kadhaa ya kesi za madai na tuhuma nzito ambapo kwa mujibu wa tovuti ya TMZ, bilionea huyo alishtakiwa kwa makosa ya njama za kihalifu, ulanguzi wa ngono, udanganyifu na usafirishaji wanawake kwa madhumuni ya ukahaba ambapo baada ya kushtakiwa, Diddy aliomba kuachiliwa kwa dhamana kabla ya kesi, lakini ombi lake lilikataliwa.

Jana Jumatano mwanzilishi huyo wa Bad Boy Records, alijitokeza tena mahakamani kusikiliza rufaa ya uamuzi wa jaji ya kutoachiwa kwa dhamana huku akionyesha utayari wake wa kutokuwa faragha yoyote na kukataa wageni wa kike nyumbani kwake kama sharti la kuachiwa kwa dhamana kabla ya kesi kusikilizwa hata hivyo, jaribio hili nalo lilikataliwa.

"Serikali imethibitisha kwamba mshtakiwa ni tishio, dhamana iliyopendekezwa haitoshi haswa kwa kuzingatia hatari ya kutoroka," alisema Jaji wa Mahakama ya Marekani Andrew Carter.

Wanawe Christian na Justin walionekana nje ya mahakama, ingawa baba yao amerudishwa mahabusu kwenye gereza la Metropolitan huko Brooklyn.
Licha ya kushindwa mara kwa mara kisheria, timu ya Diddy inaonekana kuwa na imani kuwa wataweza kumsaidia kuondokana na mashtaka hayo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags